RAIS JACOB ZUMA ASEMA HAONI SABABU YOYOTE YA KUJIUZULU



Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma amesema hajafanya makosa na haoni sababu ya kujiuzulu.

Bw.Zuma alizungumza baada ya chama tawala cha ANC kumtaka kujiuzulu vinginevyo atakabiliwa na kura isiokuwa na imani dhidi yake leo Alhamisi.
Rais Jacob Zuma wa Afrika ya kusini amesema kuwa haoni sababu ya yeye kujiuzulu
Image captionRais Jacob Zuma wa Afrika ya kusini amesema kuwa haoni sababu ya yeye kujiuzulu

Rais huyo amekuwa chini ya shinikizo ya kujiuzulu huku kukiwa na madai mengi ya ufisadi lakini amesema ANC imeshindwa kuelezea ni kwa nini ametakiwa kujiuzulu.
Bw.Zuma amesema yuko tayari kuondoka baada ya mwezi Juni lakini akapinga vile jambo hilo linavyoangaziwa kwa sasa na alisema atatoa taarifa nyengine baadaye siku ya Jumatano.
Chama cha ANC kimesema kilisikiza matamshi ya Bw.Zuma lakini kitatoa uamuzi wa hatua yake baadaye kabla ya kuzungumza.
Kiongozi wa chama hicho Jackson Mthembu alitangaza kuwa kura isiokuwa na imani dhidi ya rais itasikilizwa siku ya Alhamisi huku Cyril Ramaphosa aliyechaguliwa kuwa rais wa chama hicho mwezi Disemba akiapishwa mara moja kuwa rais wa taifa hilo.
Mkutano wa kamati kuu ya ANC ulikuwa umetangaza uamuzi wake wa kumtaka Zuma ajiuzulu siku ya Jumanne na kumpatia hadi mwisho wa siku siku ya Jumatano kujiuzulu.
Katika mahojiano,bw.Zuma hakuzungumza kuhusu uvamizi wa mapema alfajiri uliotekelezwa na maafisa wa polisi katika nyumba ya washirika wake wakuu familia ya Gupta siku ya Jumatano.
Familia ya Gupta imetuhumiwa kwa kutumia uhusiano wa karibu na rais kuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa ambapo hata hivyo pande zote mbili zimekataa kuwepo kwa madai hayo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA