MFAHAMU RAIS JACOB ZUMA AMBAYE AMEJIUZULU URAIS


 Jacob Gedleyihlekisa Zuma  alizaliwa  Aprili 12,1942. Ni Rais wa Afrika Kusini tangu 2009.Alikuwa makamu wa rais chini ya Thabo Mbeki kati ya 1999 na 2005.Tangu Desemba 2007 ni mwenyekiti wa chama tawala cha ANC.

KIJANA NA MWANAHARAKATI WA ANC

Alizaliwa kama mtoto wa wazazi maskini katika eneo la Kwa Zulu-Natal.Akiwa na umri wa miaka 17 akajiunga na ANC akaingia katika upinzani mkali dhidi ya serikali ya apartheid(ubaguzi wa rangi wa kisheria).
Mwaka 1963 alikamatwa akafungwa jela miaka 10 huko Robben Island pamoja na Nelson Mandela ambapo baada ya kuondoka gerezani akatoka Afrika Kusini akashiriki katika shughuli za nje za ANC huko Msumbiji na Zambia na aliingia katika uongozi hadi kuwa mkuu wa ujasusi wa jeshi la ANC.

KUPANDA NGAZI KATIKA AFRIKA KUSINI HURU

Tangu ANC kuhalalishwa tena nchini Afrika Kusini mwaka 1990,Zuma alikuwa mwenyekiti wa chama cha Natal na baada ya uchaguzi wa 1994 akawa waziri katika serikali ya jimbo.
Mwaka 1997 alikuwa Makamu wa Mwenyekiti wa ANC na mwaka 1999 akateuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri.

KUACHISHWA KAZI SERIKALINI 2005

Mwaka 2005 mshauri wake Shabir Shaik alihukumiwa miaka 15 jela kwa sababu alipokea rushwa.Zuma alishtakiwa pia na Rais Thabo Mbeki akamwachisha Umakamu wa Rais.Kesi hii ilisimamishwa kwa sababu mashitaka hayakuandaliwa vizuri.Kuna maandalizi ya kupeleka mashitaka mapya.
Miezi michache baadaye alishtakiwa tena kwa sababu mama mmoja alidai ya kuwa alinajisiwa na Zuma.Katika kesi hii Zuma hakuhukumiwa kwa sababu hakimu aliamini madai kwamba mama yule alikubaliana naye.

KURUDI KWAKE KAMA KIONGOZI WA ANC 2007

Mwaka 2007 Zuma akagombea nafasi ya mwenyekiti wa ANC dhidi ya Thabo Mbeki aliyetaka kuchaguliwa tena ambapo Zuma alishinda.
Na sasa tayari amejiuzulu urais leo Februari 15 baada ya kuandamwa sana na chama chake.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA