MORGAN TSVANGIRAI AFARIKI DUNIA


Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika kusini.
Kwa mujibu wa kiongozi Mwandamizi wa chama cha MDC,Tsvangirai mwenye umri wa 65,na aliyewahi kushika nafasi ya Uwaziri mkuu nchini Zimbabwe ameripotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya utumbo.
Marehemu Morgan Tsvangirai
Marehemu Morgan Tsvangirai

Makamu Rais wa chama chama cha MDC Elias Mudzuri amesema marehemu alifariki jana jioni Februar 14.
Katika kipindi cha uhai wake,maisha yake ya kazi yaligubikwa na harakati nyingi za kisiasa dhidi ya mpinzani wake Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe.
Morgan Tsvangirai alianzisha chama cha Movement for Democratic Change -MDC- mwaka 2000 na kuanza kutoa changamoto kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo aliyekaa madarakani muda mrefu.
Kufuatia kifo hicho Bw.Tsvangirai,MDC inaelekea kugawanyika juu ya nani atakayeongoza uchaguzi hapo baadaye mwaka huu dhini ya chama tawala cha Zanu PF, ambacho kwa sasa kinaongozwa na Emmerson Mnangagwa.
Bw.Tsvangirai,Aliwahi kupigwa na kufungwa mara kadhaa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA