HATIMAYE RAIS ZUMA AJIUZULU


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameamua kujiuzulu mara moja kufuatia kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa chama chake kinachotawala nchini humo cha African National Congress, ANC.
Chama tawala nchini Africa kusini cha ANC,kimepokea tangazo la kujiuzulu kwa Rais Jacob Zuma katika nafasi yake ya Urais.
Afisa mmoja mwandamizi wa chama hicho amesema hatua hiyo italeta utulivu wakati nchi inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Ameongeza kwa kusema kuwa ANC haisherehekei hatua hiyo,kutokana na kuwa Zuma amekitumikia chama hicho kwa miaka 60.
Awali kupitia televisheni Bw.Zuma alisema hakubaliani na mahitaji ya uongozi wa ANC kwamba anapaswa kujiuzulu, lakini amejiuzulu ili kuepusha ghasia ambazo zingechafua jina lake.
Makamu wa Rais wa Africa kusini Cyril Ramaphosa atapigiwa kura na wabunge kama mkuu wa nchi na baadaye kula kiapo ndani ya siku chache zijazo.
Zuma alikilalamikia chama cha ANC kwa kumtaka aondoke madarakani,ikiwa ni pamoja na kumtishia kumuondoa kupitia kura ya bunge ya kutokuwa na imani naye iliyopangwa kupigwa hii leo Alhamisi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA