Posts

Showing posts from September 7, 2017

TUNDU LISSU APIGWA RISASI APELEKWA CHUMBA CHA UPASUAJI DODOMA-Septemba 7,2017

Image
Mh.Tundu Lissu Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi nyumbani kwake na kwamba hali yake ni mbaya.

WAZIRI SIMBACHAWENE AJIUDHULU KWA AGIZO LA RAIS MAGUFULI-Septemba 7,2017

Image
Mh.George Simbachawene Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,George Simbachawene ameandika barua ya kujiudhulu wadhifa huo baada ya kutajwa katika ripoti za uchunguzi wa biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi iliyoonyesha namna serikali lilivyopoteza matrilioni ya fedha kutokana na sababu mbalimbali. Waziri Simbachawene ameandika barua hiyo muda mfupi baada ya Rais Magufuli kuwataka viongozi wote aliowateua na wametajwa katika ripoti hiyo wakae pembeni ili kupisha uchunguzi ambao utakuwa huru na wa haki. Mbali na Simbachawene,wengine waliokuwa wametakiwa kukaa pembeni ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Edwin Ngonyani ambaye alituhumiwa kutotekeleza majukumu yake kikamilifu alipokuwa akifanya kazi katika Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) lenye dhamana ya kusimamia madini. Mbali na Ngonyani,mwingine ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara,Eliakim Maswi baye naye amepaswa kupisha uchunguzi ambapo Rais ameagiza ufa

EKARI 100 ZATENGWA MKOANI RUKWA KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA-Septemba 7,2017

Image
Aliyesimama ni Mh. Bupe Mwakang'ata Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari 100 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya.

FIDIA KWA WANANCHI MKOANI KATAVI-Septemba 7,2017

Image
Mh.Roda Kunchela mbunge viti maalumu Katavi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani NAIBU waziri wa ujenzi,Uchukuzi na mawasiliano Mh.Edwin Ngonyani amesema kila mwananchi anayesitahili kupewa fidia kutokana na ujenzi wa lami kutoka Mpanda kuelekea Mkoani Kigoma atapewa fidia yake kwa mjibu wa sheria.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA KULETEWA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 700 KWA AJILI YA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA-Septemba 7,2017

Image
Mh.Suleiman Kakoso Mbunge Jimbo la Mpanda Vijijini Mh.Suleiman Jafo Naibu waziri(TAMISEMI) SERIKALI imesema imetenga zaidi ya shilingi Bilioni 700 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda iliyopo Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi hususani kituo cha afya cha majalila kilichopo makao makuu ya wilaya ya Tanganyika.

NEEMA SEKTA YA AFYA-MKOANI RUKWA-Septemba 7,2017

Image
Naibu waziri Suleiman Jafo NAIBU waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh.Suleiman Jafo amesema katika mwaka wa fedha 2017/2018 serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni   251 kwa ajili ya mkoa wa Rukwa ambapo kati ya kiasi hicho shilingi Bilioni 68 zinatarajiwa kutumika kukamilisha majengo ya vituo mbalimbali vya huduma za afya vilivyopo mkoani Rukwa.

TUMBUA TUMBUA VIGOGO WA SERIKALINI YABISHA HODI TENA-Septemba 7,2017

Image
Rais Magufuli amewataka viongozi mbalimbali wa serikali ambao wametajwa kwenye ripoti za bunge ya madini ya Almasi na Tanzanite wamepishe nafasi zao ili vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yake vizuri kuwachunguza.