NEEMA SEKTA YA AFYA-MKOANI RUKWA-Septemba 7,2017



Naibu waziri Suleiman Jafo
NAIBU waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh.Suleiman Jafo amesema katika mwaka wa fedha 2017/2018 serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni  251 kwa ajili ya mkoa wa Rukwa ambapo kati ya kiasi hicho shilingi Bilioni 68 zinatarajiwa kutumika kukamilisha majengo ya vituo mbalimbali vya huduma za afya vilivyopo mkoani Rukwa.

Waziri Jafo ametoa majibu hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu maswali ya wabunge wa mkoani Rukwa waliotaka kujua mpango wa serikali katika kuondoa changamoto mbalimbali zinazolenga sekta ya afya Mkoani Rukwa na kuwa vikwazo kwa wananchi.
Miongoni mwa changamoto hizo ambazo ni kikwazo kwa wananchi  ni pamoja uhaba wa vituo vya afya uhaba wa majengo na vyumba vya upasuaji katika hospitali.
Waziri Jafo amesema serikali imeelekeza nguvu kujenga vyumba vya upasuaji katika kituo cha afya cha Kilando kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Nkasi huku akisema kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ikitengewa shilingi Milioni 340 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kalambo.
Wakati huo huo amesema Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ipo katika hali mbaya ambapo katika utatuzi wa upungufu wa vituo vya huduma za afya serikali inaendelea kujenga Vituo vya afya vya Milepa na Mwimbe ambapo imekwishapeleka shilingi zipatazo milioni 500 ili kuanza ujenzi na uboreshaji.
Mkoa wa Rukwa unaundwa na Wilaya tatu ambazo ni Sumabawanga Nkasi na Kalambo ambazo zinahitaji kuwepo kwa vituo vya huduma za afya za kutosha katika Halmashauri 4 za mkoa huo ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda,Halmashauri ya wilaya ya Mpanda,Nkasi na Kalambo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA