EKARI 100 ZATENGWA MKOANI RUKWA KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA-Septemba 7,2017



Aliyesimama ni Mh.Bupe Mwakang'ata
Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari 100 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya.

Kwa sasa taratibu za ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi huo zinakamilika na serikali itawalipa fidia stahiki wahusika.
Akijibu swali bungeni leo,Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo  amesema kwa sasa wagonjwa wanapata huduma katika hospitali teule iliyopo pamoja na vituo vya Afya na zahanati.
Katika swali la msingi, mbunge wa viti maalumu Bupe Mwakang'ata  (Chadema), ametaka kujua  ni lini serikali itajenga hospitali ya wilaya katika wilaya za Nkasi na Sumbawanga ambako wanawake wanapata shida.
"Serikali itajitahidi kutafuta fedha na kushirikiana na wananchi wa Nkasi ili kufanikisha ujenzi wa hospitali ya wilaya," amesema Jafo.
Kuhusu hospitali ya rufaa alisema Mkoa wa Rukwa umeanza taratibu za ujenzi wa hospitali katika eneo la Milanzi ambapo hospitali inayotumika kwa sasa itabaki kuwa hospitali ya wilaya ya Sumbawanga.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA