HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA KULETEWA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 700 KWA AJILI YA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA-Septemba 7,2017



Mh.Suleiman Kakoso Mbunge Jimbo la Mpanda Vijijini
Mh.Suleiman Jafo Naibu waziri(TAMISEMI)
SERIKALI imesema imetenga zaidi ya shilingi Bilioni 700 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda iliyopo Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi hususani kituo cha afya cha majalila kilichopo makao makuu ya wilaya ya Tanganyika.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni Dodoma na Naibu waziri wa Tawala za mikoa na Serikali za mitaa(TAMISEMI) Mh.Suleiman Jafo wakati akijibu swali la mbunge wa Jimbo la Mpanda vijijini Mh.Suleiman Moshi Kakoso aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu kutoa pesa kwa ajili ya kituo cha afya cha Majalila.
Mh.Jafo amesema kati ya shilingi bilioni 700 ziazotarajiwa kuletwa wilayani Tanganyika,zaidi ya shilingi bilioni 200 ni kwa ajili ya kununua vifaa tiba katika vituo vya vya huduma za afya vilivyopo wilayani Tanganyika.
Agosti 16 mwaka huu serikali kupitia kwa naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii jinsia,Wazee na Watoto Mh.Ummy Mwalimu ilisema inatarajia kuelekeza nguvu kubwa katika kujenga na kuboresha huduma za afya mkoani katavi ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Mkoani wa Katavi pamoja na ujenzi wa benki ya damu salama ili wananchi wapate huduma zilizobora.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA