Posts

Showing posts from March 28, 2018

IGP SIRRO AWAHAKIKISHIA USALAMA WATANZANIA WOTE KIPINDI CHA PASAKA

Image
Amesema Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro matukio  makubwa ya uhalifu wa kutumia Silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini. IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari ili kutoa salaamu za pasaka kwa watanzania ambapo amewashukuru Wananchi kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa Jeshi la Polisi  jambo ambalo limesaidia kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa hapa nchini.  Aidha amesema jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea ili  kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia. Katika hatua nyingine amesema jeshi la Polisi katika mikoa yote linawahakikishia wananchi kuwa limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa sikukuu hii inasherekewa kwa amani na utulivu na hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyofanyika na vitakapojitokeza vitadhibitiwa kwa haraka. Ulinzi utaimarishwa kwenye maeneo yote yakiwemo maeneo ya kuabudia,fukwe,sehemu za starehe n

DKT.SHEIN AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Viongozi walioapishwa na Rais Dk.Shein katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ni Fatma Gharib Bilal ambaye ameapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee, Wanawake na Watoto na Abdalla Hassan Mitawi ambaye ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid,Jaji Mkuu wa Zanzibar   Omar Othman Makungu,Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said pamoja na Mawaziri. Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih,Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,Mkuu wa   Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud,Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine

RIPOTI YA DAKTARI KUHUSU WALIOKUFA KWA SUMU YA UYOGA KATAVI HII HAPA

Image
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Dkt. Theopister Elisa amesema uchunguzi wa kitabibu unaonesha mwanamke Mariana Gerald Sanane(47) mkazi wa kijiji cha Sitalike Wilayani Mpanda aliyefariki duniani baada ya kula uyoga unaotajwa kuwa na sumu aliathiriwa katika ini. Dkt.Theopister Elisa ameeleza hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari kueleza walichokibanini kwa mwanamke huyo baada ya kufariki kwa kula uyoga ambao unadaiwa kuchumwa kutoka zizi la ng’ombe baada ya uyoga huo kumwagiwa dawa ya kupulizia ng’ombe. Aidha Dkt.Elisa amesema waathiriwa wa sumu hiyo walicheleweshwa kufikishwa katika vituo vya huduma za afya hali iliyosababisha mathara makubwa kujitokeza mwilini mpaka kusababisha mauti baada ya idi kuathirika. Machi 25 mwaka huu Frenki Mayaga na Erizabeth George wakazi kijiji cha Sitalike wakiwa wa familia moja,walifariki dunia baada ya kula uyoga huo wenye sumu na hivyo kufikisha idadi ya watu watatu waliofariki dunia wote wakitoka katik