RIPOTI YA DAKTARI KUHUSU WALIOKUFA KWA SUMU YA UYOGA KATAVI HII HAPA


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Dkt. Theopister Elisa amesema uchunguzi wa kitabibu unaonesha mwanamke Mariana Gerald Sanane(47) mkazi wa kijiji cha Sitalike Wilayani Mpanda aliyefariki duniani baada ya kula uyoga unaotajwa kuwa na sumu aliathiriwa katika ini.
Dkt.Theopister Elisa ameeleza hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari kueleza walichokibanini kwa mwanamke huyo baada ya kufariki kwa kula uyoga ambao unadaiwa kuchumwa kutoka zizi la ng’ombe baada ya uyoga huo kumwagiwa dawa ya kupulizia ng’ombe.
Aidha Dkt.Elisa amesema waathiriwa wa sumu hiyo walicheleweshwa kufikishwa katika vituo vya huduma za afya hali iliyosababisha mathara makubwa kujitokeza mwilini mpaka kusababisha mauti baada ya idi kuathirika.
Machi 25 mwaka huu Frenki Mayaga na Erizabeth George wakazi kijiji cha Sitalike wakiwa wa familia moja,walifariki dunia baada ya kula uyoga huo wenye sumu na hivyo kufikisha idadi ya watu watatu waliofariki dunia wote wakitoka katika familia hiyo.
Hata hivyo Dkt.Elisa amesema mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 60 aliruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupatiwa matibabu.
Kwa mjibu wa mwenyekiti wa kijiji cha Sitalike Bw.Christopher Anjero,tukio hilo la kusikitisha halijatokea katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi iliyopita.
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANI.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA