IGP SIRRO AWAHAKIKISHIA USALAMA WATANZANIA WOTE KIPINDI CHA PASAKA


Amesema Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro matukio  makubwa ya uhalifu wa kutumia Silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini.
IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari ili kutoa salaamu za pasaka kwa watanzania ambapo amewashukuru Wananchi kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa Jeshi la Polisi  jambo ambalo limesaidia kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa hapa nchini. 
Aidha amesema jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea ili  kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia.
Katika hatua nyingine amesema jeshi la Polisi katika mikoa yote linawahakikishia wananchi kuwa limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa sikukuu hii inasherekewa kwa amani na utulivu na hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyofanyika na vitakapojitokeza vitadhibitiwa kwa haraka.
Ulinzi utaimarishwa kwenye maeneo yote yakiwemo maeneo ya kuabudia,fukwe,sehemu za starehe na sehemu zenye mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo katika hali ya  utulivu.
Kwa upande wa wazazi wametakiwa kuwaangalia watoto wao na kutowaacha kutembea peke yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu pia wamiliki wa kumbi za starehe wanatakiwa  kufuata sheria,kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo ikiwemo kutoruhusu disko toto na kujaza watu kupita kiasi.
Vilevile Jeshi la Polisi linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa makini na kuzingatia Sheria za Usalama barabarani hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kujaza watu kupita kiasi,kubeba mishikaki,kwenda mwendo kasi,kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.
Habari kamili ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM   

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA