Posts

Showing posts from January 6, 2018

ANAYEJIHUSISHA NA UUZAJI VIUNGO VYA BINADAMU ADAKWA NA POLISI NCHINI CYPRUS,KUFIKISHWA MAHAKAMANI

Polisi nchini Cyprus wamesema wanamshikilia raia mmoja wa Israel Moshe Harel anayetuhumiwa kufanya biashara ya viungo vya binadam. Harel amehusishwa kufanya biashara ya figo kwa matariji wa Israel takriban miaka kumi sasa. Amehusishwa kuchukua figo za raia wa Kosovo pamoja na Uturuki na nchi nyingine kadhaa ambao mpaka sasa hajawalipa chochote. Msemaji wa polisi nchini Cyprus amesema mtu huyo alikamatwa uwanja wa ndege wa Larnaca mwezi Desemba mwaka jana ambapo anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumanne ya wiki ijayo kujibu mashtaka yanayomkabili. Wakati huo hupo Harel anahitajika kwa makosa kama hayo nchini Kosovo ili kujibu tuhuma zinazomkabili. Chanzo:bbc Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WABUNGE WALIOJIUZULU VYAMA VYA UPINZANI NA KUJIUNGA CCM WAPITISHWA KUGOMBE KATIKA MAJIMBO YAO

Image
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewarudisha waliokuwa wabunge wa upinzani kugombea majimbo ya Siha na Kinondoni baada ya wabunge hao kuijiunga na chama hicho. Uthibitisho huo umeelezwa katika taarifa ambayo imetolewa leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Hamphrey Polepole imesema,baada ya tafakuri na tathimini ya kina. Polepole amesema Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM na kwa mamlaka iliyokasimiwa kwake na Kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) imemteua Dk Godwin Mollel kusimama na kugombea Jimbo la Siha Mkoani Kilimanjaro na Maulid Mtulia kusimama na kugombea Jimbo la Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam. NEC imesema wagombea wa ubunge wanaelekezwa kufika katika ofisi za CCM katika mikoa husika na kupokea maelekezo yahusuyo uchaguzi kutoka kwa makatibu wa CCM wa mikoa hiyo Jumanne ijayo ya Januari 9 bila kukosa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MWANASIASA MKONGWE KINGUNGE APOKEA KWA MASIKITIKO KIFO CHA MKEWE

Image
Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru leo amepewa taarifa za kifo cha mke wake Pares Mwiru ambazo imeelezwa kuwa amezipokea kwa mshtuko mkubwa. Kingunge ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi ya Mwaisela akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Kijitonyama,alifanyiwa upasuaji Januari 4 mwaka huu. Mtoto wa mwanasiasa huyo Kinje Mwiru amesema wamempa taarifa baba yao saa tano asubuhi leo huku Kinje akisema kwa sasa wamemuacha baba yake apumzike ili aweze kuwapatia mwongozo nini kifanyike baada ya kifo cha mke wake. Pares alifariki Januari 4 saa nane mchana katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa tangu alipofikishwa Muhimbili Oktoba 3,mwaka jana. Kwa mjibu wa Ofisa Uhusiano wa MNH John Stephen amesema kwa sasa afya ya mwanasiasa huyo mkongwe imeimarika. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WAZIRI MKUU AAGIZA VYAMA VIWILI VICHUNGUZWE

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amebaini Kasoro nyingi katika Vyama Vikuu vya Ushirika vya Mbinga (MBICU na MBIFACU) na kuagiza uchunguzi ufanyike. Majaliwa ametoa agizo hilo wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mbinga katika viwanja vya CCM,mjini Mbinga ambapo amesema timu ya uchunguzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu itakiangalia chama hicho na kukifumua chote. Kwa upande mwingine Waziri Mkuu amewaamuru  viongozi wote wa zamani na wa sasa waripoti kwa Mkuu wa Wilaya huku  OCD akihakikisha ofisi za vyama hivyo hazifunguliwi hadi kazi ya uchunguzi itakapoanza ili kuepuka kubadilisha nyaraka katika ofisi zao. Aidha Mh.Majaliwa amesema wote watakaobainika kuhusika katika kasoro hizo watachukuliwa hatua za kinidhamu. Waziri Mkuu pia ameeleza kuwa Serikali imeamua kuboresha ufanisi katika mazao matano ya biashara ambayo ni Pamba, Kahawa,Chai,Korosho na Tumbaku kwa sababu yanaliingizia Taifa fedha za kigeni. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RAIS MAGUFULI ATEMBELEA WAGONJWA HOSPITALI YA TAIOFA MUHIMBILI WAKWEMO KINGUNGE NA MAPACHA WALIOUNGANA

Image
Mapacha walioungana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli leo amewajulia hali baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam wakiwemo Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na Mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti. Katika wodi ya Mwaisela,Mhe.Rais Magufuli amemjulia hali Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ambaye anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa wake nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Kingunge Mwiru Dkt.Ibrahim Mkoma wa hospitali hiyo amemueleza Mhe.Rais Magufuli kuwa hali ya Mzee Kingunge inaendelea vizuri ambapo Mzee Kingunge amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa kumwona hospitalini hapo na amemueleza kuwa sasa anajisikia nafuu baada ya kupata matibabu. Pamoja na kumpa pole na kumuombea apone haraka,Mhe.Rais Magufuli amesema anatambua mchango mkubwa wa Mzee Kingunge katika siasa na maendeleo ya nchi. Rais pia Katika wodi ya Sewahaji,amemjulia hali Bw.Ric

MAMLUKI WADAIWA KUINGIZWA UGAWAJI WA VIWANJA KWA WAKAZI WA MSASANI NA TAMBUKARELI MKOANI KATAVI

Na.Issack Gerald Wakazi wengi wa Mtaa wa Msasani na Tambukareli Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi hawajahama kupisha mipaka ya hifadhi ya reli licha ya kutakiwa kuondoka kabla ya mwezi Januari mwaka huu. Wakizungumza kwa Nyakati tofauti wamesema,baadhi yao wamesema hawajaondoka katika maeneo hayo kutokana na ukosefu wa viwanja huku wakisema baadhi ya wajumbe wa serikali ya mtaa huo wamejigawia kiwanja zaidi ya kimoja kinyume na utaratibu ulivyopangwa. Kwa upande wake mwenyekiti wa Mtaa wa Msasani Jonard Makoli amekanusha wajumbe wa serikali kujipatia viwanja zaidi ya kimoja ambapo amesema mchakato wa majina ya wanaotakiwa kupata viwanja ilipitia katika vikao na mikutano ya hadhara. Wakati huo huo Makoli amesema Manispaa ya Mpanda kuchelewa kupima viwanja kumesababisha zaidi ya wakazi 200 kukosa viwanja vya kujengea makazi yao mpaka sasa. Hata hivyo Bw.Makoli amesema kamati iliyokuwa inafuatilia rufaani inayopinga bomoabomoa haijajulikana ni lini itatoa taarifa rasmi ya hatua

CWT KATAVI CHAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KUTENGA SHILINGI BIL.200 KULIPA MADENI YA WATUMISHI

Chama cha Walimu CWT mkoa wa Katavi kimempongeza rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa kutangaza kutoa fedha Shilingi bilioni 200 ili zilipe madeni ya ndani yakiwemo ya walimu. Kauli ya pongezi imetolewa na katibu wa chama hicho mwalimu Hamis Chinahova ambapo amesema hatua ya serikali kulipa madeni hayo italeta mageuzi makubwa katika sekta ya elimu. Katika hatua nyingine amewataka waalimu kuendelea kujituma na kufanya kazi kwa weledi zaidi ili kuleta tija kwa jamii na taifa kwa ujumla. Mwaka 2017 walimu nchini Tanzania walitishia kugoma kwa kile walichokitaja kuwa ni kukithiri kwa madai dhidi ya serikali wakisema inawavunja molali ya kufanya kazi. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MATUKIO 18742 YALITIKISA MKOANI KATAVI KWA MWAKA 2017

Jeshi la Polisi Mkoani Katavi limesema makosa 18742 ya kiuharifu yameripotiwa katika kipindi cha mwezi Januari mpaka Desemba mwaka 2017. Akitoa ripoti ya mwaka 2017 kuhusu hali ya usalama,Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda amesema utofauti wa matukio ya uhalifu kati ya mwaka 2017 na 2016 ni 1101 ambapo kwa mwaka 2016 kulikuwa na matukio 17641 yaliyoripotiwa katika vituo vya polisi. Kamanda Nyanda amesema matukio yaliyochukua nafasi kubwa yanahusu usalama barabarani mwaka 2017 yaliripotiwa matukio 11592 sawa na asilimia 62 ya matukio yote huku ajali zikiwa 55 kwa mwaka 2017 na 65 kwa mwaka 2016. Aidha Kamanda Nyanda amesema matukio ya Jinai yaliyoripotiwa Kwa kipindi cha Januari mpaka Desember 2017 ni 7150 ikilinganishwa na matukio 7549 yaliyoripotiwa kwa kipindi cha mwaka 2016 na kuwa na upungufu wa matukio ya jinai 399 sawa na asilimia 5.3 ya matukio yote. Amesema matukio makubwa 901 ya Jinai yaliripotiwa kwa kipindi cha mwaka 2017 ambapo mwaka 2016 kuliripotiwa

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI NAIBU WAZIRI WA MADINI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli leo amemteua Mhe.Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini. Mhe.Biteko ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe na alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya muda iliyochunguza madini ya Tanzanite. Kufuatia uteuzi huo,Wizara ya Madini sasa itakuwa na Waziri na Naibu Mawaziri wawili. Kwa mjibu wa taarifa ambayo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya rais Ikulu Gerson Msigwa amesema, rais Magufuli amefanya uteuzi huu kwa lengo la kuongeza nguvu kutokana na uwingi wa majukumu katika Wizara ya Madini. Mhe.Doto Mashaka Biteko anatarajiwa kuapishwa Jumatatu Januari 08 Januari mwaka huu Ikulu Jijini Dar es Salaam. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED