WAZIRI MKUU AAGIZA VYAMA VIWILI VICHUNGUZWE

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amebaini Kasoro nyingi katika Vyama Vikuu vya Ushirika vya Mbinga (MBICU na MBIFACU) na kuagiza uchunguzi ufanyike.
Majaliwa ametoa agizo hilo wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mbinga katika viwanja vya CCM,mjini Mbinga ambapo amesema timu ya uchunguzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu itakiangalia chama hicho na kukifumua chote.
Kwa upande mwingine Waziri Mkuu amewaamuru  viongozi wote wa zamani na wa sasa waripoti kwa Mkuu wa Wilaya huku  OCD akihakikisha ofisi za vyama hivyo hazifunguliwi hadi kazi ya uchunguzi itakapoanza ili kuepuka kubadilisha nyaraka katika ofisi zao.
Aidha Mh.Majaliwa amesema wote watakaobainika kuhusika katika kasoro hizo watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Waziri Mkuu pia ameeleza kuwa Serikali imeamua kuboresha ufanisi katika mazao matano ya biashara ambayo ni Pamba, Kahawa,Chai,Korosho na Tumbaku kwa sababu yanaliingizia Taifa fedha za kigeni.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA