RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI NAIBU WAZIRI WA MADINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli leo amemteua Mhe.Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini.
Mhe.Biteko ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe na alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya muda iliyochunguza madini ya Tanzanite.
Kufuatia uteuzi huo,Wizara ya Madini sasa itakuwa na Waziri na Naibu Mawaziri wawili.
Kwa mjibu wa taarifa ambayo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya rais Ikulu Gerson Msigwa amesema, rais Magufuli amefanya uteuzi huu kwa lengo la kuongeza nguvu kutokana na uwingi wa majukumu katika Wizara ya Madini.
Mhe.Doto Mashaka Biteko anatarajiwa kuapishwa Jumatatu Januari 08 Januari mwaka huu Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA