ANAYEJIHUSISHA NA UUZAJI VIUNGO VYA BINADAMU ADAKWA NA POLISI NCHINI CYPRUS,KUFIKISHWA MAHAKAMANI

Polisi nchini Cyprus wamesema wanamshikilia raia mmoja wa Israel Moshe Harel anayetuhumiwa kufanya biashara ya viungo vya binadam.
Harel amehusishwa kufanya biashara ya figo kwa matariji wa Israel takriban miaka kumi sasa.
Amehusishwa kuchukua figo za raia wa Kosovo pamoja na Uturuki na nchi nyingine kadhaa ambao mpaka sasa hajawalipa chochote.
Msemaji wa polisi nchini Cyprus amesema mtu huyo alikamatwa uwanja wa ndege wa Larnaca mwezi Desemba mwaka jana ambapo anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumanne ya wiki ijayo kujibu mashtaka yanayomkabili.
Wakati huo hupo Harel anahitajika kwa makosa kama hayo nchini Kosovo ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Chanzo:bbc

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA