MAMLUKI WADAIWA KUINGIZWA UGAWAJI WA VIWANJA KWA WAKAZI WA MSASANI NA TAMBUKARELI MKOANI KATAVI

Na.Issack Gerald
Wakazi wengi wa Mtaa wa Msasani na Tambukareli Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi hawajahama kupisha mipaka ya hifadhi ya reli licha ya kutakiwa kuondoka kabla ya mwezi Januari mwaka huu.
Wakizungumza kwa Nyakati tofauti wamesema,baadhi yao wamesema hawajaondoka katika maeneo hayo kutokana na ukosefu wa viwanja huku wakisema baadhi ya wajumbe wa serikali ya mtaa huo wamejigawia kiwanja zaidi ya kimoja kinyume na utaratibu ulivyopangwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Mtaa wa Msasani Jonard Makoli amekanusha wajumbe wa serikali kujipatia viwanja zaidi ya kimoja ambapo amesema mchakato wa majina ya wanaotakiwa kupata viwanja ilipitia katika vikao na mikutano ya hadhara.
Wakati huo huo Makoli amesema Manispaa ya Mpanda kuchelewa kupima viwanja kumesababisha zaidi ya wakazi 200 kukosa viwanja vya kujengea makazi yao mpaka sasa.
Hata hivyo Bw.Makoli amesema kamati iliyokuwa inafuatilia rufaani inayopinga bomoabomoa haijajulikana ni lini itatoa taarifa rasmi ya hatua iliyofikia katika kipindi cha mwaka 2018 ambapo mara ya mwisho kamati ilitakiwa kukamilisha malipo ya ada ya rufaani mwezi Novemba mwaka jana.
Zaidi ya wakazi 280 wa mitaa ya Msasani na Tambukareli wameathiriwa na tangazo la bomoabomoa lililotolewa na mwishoni mwa mwaka jana na mamlaka inayohusika na reli Tanzania.
Hata hivyo huenda Shirika la reli Tanzania TRL likaanza kuendesha bomoabomoa kwa kuwa muda uliotolewa kwa wakazi hao kuishi katika maeneo hayo ulikwisha Tangu mwezi Desemba mwaka jana.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA