MWANASIASA MKONGWE KINGUNGE APOKEA KWA MASIKITIKO KIFO CHA MKEWE

Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru leo amepewa taarifa za kifo cha mke wake Pares Mwiru ambazo imeelezwa kuwa amezipokea kwa mshtuko mkubwa.
Kingunge ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi ya Mwaisela akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Kijitonyama,alifanyiwa upasuaji Januari 4 mwaka huu.
Mtoto wa mwanasiasa huyo Kinje Mwiru amesema wamempa taarifa baba yao saa tano asubuhi leo huku Kinje akisema kwa sasa wamemuacha baba yake apumzike ili aweze kuwapatia mwongozo nini kifanyike baada ya kifo cha mke wake.
Pares alifariki Januari 4 saa nane mchana katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa tangu alipofikishwa Muhimbili Oktoba 3,mwaka jana.
Kwa mjibu wa Ofisa Uhusiano wa MNH John Stephen amesema kwa sasa afya ya mwanasiasa huyo mkongwe imeimarika.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA