MATUKIO 18742 YALITIKISA MKOANI KATAVI KWA MWAKA 2017

Jeshi la Polisi Mkoani Katavi limesema makosa 18742 ya kiuharifu yameripotiwa katika kipindi cha mwezi Januari mpaka Desemba mwaka 2017.
Akitoa ripoti ya mwaka 2017 kuhusu hali ya usalama,Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda amesema utofauti wa matukio ya uhalifu kati ya mwaka 2017 na 2016 ni 1101 ambapo kwa mwaka 2016 kulikuwa na matukio 17641 yaliyoripotiwa katika vituo vya polisi.
Kamanda Nyanda amesema matukio yaliyochukua nafasi kubwa yanahusu usalama barabarani mwaka 2017 yaliripotiwa matukio 11592 sawa na asilimia 62 ya matukio yote huku ajali zikiwa 55 kwa mwaka 2017 na 65 kwa mwaka 2016.
Aidha Kamanda Nyanda amesema matukio ya Jinai yaliyoripotiwa Kwa kipindi cha Januari mpaka Desember 2017 ni 7150 ikilinganishwa na matukio 7549 yaliyoripotiwa kwa kipindi cha mwaka 2016 na kuwa na upungufu wa matukio ya jinai 399 sawa na asilimia 5.3 ya matukio yote.
Amesema matukio makubwa 901 ya Jinai yaliripotiwa kwa kipindi cha mwaka 2017 ambapo mwaka 2016 kuliripotiwa matukio 973 na kuwa na upungufu wa matukio 72 sawa na asilimia 7.4 ya matukio yote makubwa ya jinai.
Katika hatua nyingine taarifa ya Kamanda Nyanda inaonesha Jumla ya silaha 09 zikiwemo SMG 02 na Gobore 07 zilisalimishwa kwa mwaka 2016 huku kwa mwaka 2017 jumla ya silaha 16 zikiwemo SMG 05,Short gun 02 na Gobore 12 zikisalimishwa.
Katika hatua nyingine katika kipindi cha mwaka 2017 jeshi la polisi limetembelea vijiji vyote 177 mkoani katavi huku katika kipindi cha mwaka 2018 wakitarajia kutembelea vitongoji vyote 933 ili kutoa elimu ya polisi jamii kwa wananchi.
Hata hivyo kuanzia Januari 28 mpaka 30 mwaka huu,jeshi la polisi linatarajia kuendesha zoezi la uwekaji wa alama maalumu ya utambulisho wa silaha za kiraia na kuwataka wamiliki wote wa silaha za kiraia kufika kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA