FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM



Jokate Mwegelo

Jokate Mwegelo
Amezaliwa
Jokate Urban Mwegelo
20 Machi 1987 (umri 31)
20 Machi 1987 (umri 31)
Utaifa
Kazi yake
Mwigizaji, mjasiriamali, mtangazaji, mwimbaji
Miaka ya kazi
2006-hadi sasa
Jokate Mwegelo ni mwigizaji wa filamu na mjasiriamali kutoka nchini Tanzania. Jokate vilevile ni mtangazaji na mwimbaji.
Huyu ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Kidoti Company.Mwaka wa 2011,alishinda tuzo ya Zanzibar International Film Festival akiwa kama mwigizaji bora filamu wa kike.Mwaka wa 2017,Mwegelo aliingizwa katika jarida la Forbes katika Forbes 30 Under 30 kutoka Afrika.

MAISHA YA AWALI NA ELIMU.

Mwegelo alizaliwa mnamo tarehe 20 Machi,1987 huko mjini Washington D.C ambapo wakati huo wazazi wake walikuwa wanafanya kazi.Alikulia jijini Dar es Salaam, Tanzania.Alianza elimu ya msingi katika shule ya Olympio Primary School na baadaye St.Anthony High School, halafu Loyola High School,Dar Es Salaam,Tanzania. Alihitimu katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ambapo alipata shahada ya sayansi ya siasa na falsafa.

MISS TANZANIA 2006

Alikuwa mshindi wa pili katika shinda la Miss Tanzania mwaka 2006.Vilevile alipewa jina la balozi wa Redds fashion na balozi wa gazeti la Citizen,baada ya kupata kura nyingi mwaka huo.Kabla ya Miss Tanzania, alishindana katika Miss Kurasini 2006,shindano ambalo alishinda kisha kuelekea juu zaidi na kuwa Miss Temeke 2006 ambako pia alishinda.

KAZI

Kuigiza

Mwaka wa 2007,alipata kucheza filamu yake ya kwanza iliyojulikana kwa jina la Fake Pastors,akiwa na Vincent Kigosi,Lisa Jensen,mshindi wa tatu wa Miss Tanzania 2006 na marehemu Adam Kuambiana.Mwaka wa 2008, amecheza katika filamu ya From China With True Love.Mwaka wa 2010,alionekana katika filamu ya Chumo,filamu iliyoandaliwa na Media for Development International, kuhusu elimu juu ya ugonjwa wa malaria. Filamu hii ilimwezesha kupata tuzo ya Zanzibar International Film Festival akiwa kama mwigizaji bora wa kike kwa 2011 na kuchaguliwa kama mwigizaji wa Pan-Afrika katika tuzo za 2012 Nigeria Entertainment Awards. Vilevile amepata kuonekana katika mfululizo wa TV maarufu wa Siri Ya Mtungi,uliokuwa unaandaliwa na Jordan Riber na kuongozwa na Karabani, mnamo 2013.Mwaka wa 2014, amecheza uhusika wa "Ndekwa" katika filamu ya Mikono Salama,ambayo ilimpelekea apate tuzo nyingine ya Zanzibar International Film Festival akiwa mwigizaji bora wa kike kwa filamu za Kiswahili.

Kampuni ya Kidoti

Muziki

Alishirikishwa katika wimbo wa Japo Nafasi wa Cpwaa akiwa na A.Y. katika wimbo wa Kings and Queen na Amani,kutoka Kenya.Mwaaka wa 2013, alitoa wimbo wake akiwa na Lucci,uliyoitwa 'Kaka na Dada.Mwaka wa 2015 akadondosha wimbo wake mwingine uliyoitwa Leo akiwa na mwimbaji mwingine kutoka nchini Nigeria maarufu kama Ice Prince.

Miezi 11 iliyopitia aliteuliwa na UVCCM kuwa Kaimu Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM Taifa. 
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com  

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA