MAASKOFU WAANZA KUTEMA CHECHE SUALA LA KATIBA MPYA NA USALAMA WA TAIFA


Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dk.Fredrick Shoo amesema kama taifa linahitaji maendeleo ya kweli basi kuna haja ya kuwa na katiba mpya na si iliyopo sasa. 
Askofu Dk.Fredrick Shoo 
Askofu Dk Fredrick Shoo alisema hayo baada ya kutoa ujumbe wa Pasaka na kusema kuna haja ya kuwa na katiba mpya ili kuweza kupata maendeleo ya kweli kwani katiba mpya ndiyo inaweza kuongoza kila raia. 
"Katiba iongoze kila raia, utaratibu wa Watanzania kuweza kuishi pamoja na kama tunataka maendeleo ya kweli pasipo Katiba mpya tutakuwa tunajidanganya" alisema Askofu Shoo 
Mbali na hilo Askofu Shoo aliweza kuzungumzia mambo mengi kuhusu usalama wa nchi na watu wake na kuonyesha wasiwasi kuwa kuna vitu haviendi sawa kutokana na kuibuka kwa mambo ambayo si utamaduni wa Tanzania, kama watu kupigwa risasi, kuokotwa kwa miili ya watu baharini, kuuwawa kwa watu katika mazingira ya kutatanisha.
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM   


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA