UYOGA WAUA WAWILI KATAVI NA WENGINE MAHUTUTI

Watu wawili ambao wametambulika kwa majina Frenki Mayaga na Erizabeth George wakazi wa kijiji cha  Stalike wilayani Mpanda mkoani Katavi,wafamefariki dunia baada ya kula uyoga unaotajwa kuwa na Sumu.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Christopher  Anjero amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo leo ambapo amesema mbali na marehemu hao,watu wengine watatu wako mahututi na wanaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya Mpanda.
Bi.Monica George ambaye ni miongoni mwa ndugu wa marehemu amesema walikwenda porini kutafuta uyoga ambapo baada ya kupika na kula ndiyo wakapatwa na mauti hayo.
Aidha George Anjero Mrisho amesema alipokea taarifa za kifo cha kijana wake Frenki Mayaga akiwa shambani.
Hata hivyo Mganga wa zamu wa hospitali ya Manispaa ya Mpanda hakuupatikana ili kujua taratibu za kitabibu zinazoendelea kwa sababu hakuwepo kituoni.
Kwa mjibu wa mwenyekiti wa kijiji cha Sitalike Bw. Christopher  Anjero hilo ni tukio la kwanza katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ndani ya uongozi wake.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA