Posts

Showing posts from February 25, 2016

MAFUNZO YA SIKU 3 KUHUSU UTUNZAJI WA FEDHA NA MALI ZA UMMA KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA YAANZA KATAVI.

Image
Na.Issack Gerald-Katavi MAHAKAMA ya Tanzania    imeanza   mafunzo ya siku 3   kuanzia leo hadi February 27 juu ya utunzaji wa fedha na mali ya umma kwa watumishi wa mahakama ya Tanzania mkoani Katavi katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mpanda.                                                  

MTOTO MWENYE MIAKA 03 AUWAWA KIFO CHA UTATA KATAVI,WAZAZI WAKAA NA MAITI NDANI YA NYUMBA KWA SIKU 4,MAJIRANI WARIPOTI TUKIO POLISI BAADA YA KUKERWA NA HARUFU MBAYA

Image
Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi WATU wawili ambao ni wazazi wa mtoto aliyefahamika kwa jina la Justina Laurent (3) wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Katavi kwa kusababisha kifo cha mtoto huyo ambaye aligundulika akiwa amefariki dunia ndani ya chumba cha wazazi wake huku akiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.

ZOEZI LA KUWAFILISI WENYE MAKONTENA KUANZA LEO.

Image
WADAIWA 16 waliokwepa kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), baada ya kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, mali zao zinaanza kukamatwa leo na kufilisiwa.                                                         Baadhi ya Makontena yaliyokamatwa bandarini

BAJETI IJAYO KUTEKELEZWA KWA MAPATO YA NDANI.

Image
SERIKALI imesema bajeti ya mwaka ujao, hususani utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo, itatekelezwa kwa fedha za ndani. Waziri wa fedha na Mipango Dk.Philip Mpango

CHUO KIKUU MTAKATIFU JOSEPH TAWI LA ARUSHA WAGOMA,WAKODI MABASI MATAtU KWENDA DAR ES SALAAM KUMWOMA WAZIRI NDALICHAKO.

Image
WANAFUNZI 1,548 wa Chuo Kikuu cha St. Joseph tawi la Arusha, wamegoma kuingia darasani kwa siku tatu na kukodi mabasi matatu kwenda Dar es Salaam kumwona Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako .                                                    Katibu mtendaji wa TCU Prof.Yunus Mgaya

GESI YAGUNDULIKA BONDE LA MTO RUVU

Image
TANZANIA imedhihirisha kuwa ni tajiri mkubwa wa rasilimali ya gesi asilia baada ya kugundulika kwa gesi nyingine katika bonde la mto Ruvu yenye ukubwa wa ujazo wa futi trilioni 2.17.                                                  Baadhi ya wakazi katika bonde la mto Ruvu

MAHAKAMA YAAMURU NDOA KUVUNJIKA WILAYANI MPANDA,WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SHAMBULIO LA MWILI.

Image
Na.Boniface Mpagape-Mpanda MAHAKAMA ya Mwanzo mjini Mpanda juzi imeamuru mdai Leticia Seleman awe na uhuru wa kuishi peke yake au kuanzisha mahusiano mengine ya ndoa katika kesi ya madai ya talaka kutoka kwa aliyekuwa mmewe Makono Brash.                                                   Mahakamani

BENKI YA DUNIA KUFADHIRI UJENZI WA KILOMITA 7.7 ZA BARABARA MANISPAA YA MPANDA 2016/2017

Image
Na.Issack Gerald-Mpanda Zaidi ya kilometa 7.7 za barabara katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ,zimetengwa kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami   kwa mwaka wa fedha 2016/2017.                                            Benki ya dunia

MKUU WA WILAYA MPANDA ATOA SIKU SABA KWA OFISI YA MADINI KUTATUA MGOGORO KATI YA KAMPUNI YA KIJANI INVESTMENT NA WACHIMBAJI WADOGO MPANDA.

Image
Na.Meshack Ngumba-Mpanda MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bwana   Pazza Mwamlima ametoa siku saba Kwa ofisi ya Madini Wilayani Mpanda Kutatua Mgogoro uliopo baina ya Kampuni ya Kijani Investment na Wachimbaji wadogo wa dhahabu Katika Machimbo ya Dilifu.                                              Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw.Pazza Mwamlima Akizungumza na wananchi waishio katika mgodi wa dhahabu wa Dirifu ambao kipato kikuu wanategemea mgodi huo (PICHA NA Issack Gerald)