MAHAKAMA YAAMURU NDOA KUVUNJIKA WILAYANI MPANDA,WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SHAMBULIO LA MWILI.


Na.Boniface Mpagape-Mpanda
MAHAKAMA ya Mwanzo mjini Mpanda juzi imeamuru mdai Leticia Seleman awe na uhuru wa kuishi peke yake au kuanzisha mahusiano mengine ya ndoa katika kesi ya madai ya talaka kutoka kwa aliyekuwa mmewe Makono Brash.
                                                 
Mahakamani

Akisoma hukumu hiyo, hakimu wa mahakama hiyo Bw. David Mbembela amesema mahakama imeona mdai Bi. Leticia Seleman hastahili kupewa talaka baada ya kushindwa kuithibitishia mahakama kama kuna ndoa inaendelea kati yao.
Madai hayo ya talaka yanatokana na Mdai Bi. Leticia Seleman kutaja sababu ambazo ni pamoja na kutelekezwa kwa muda mrefu, kutishiwa kuuawa na kwamba mdaiwa Bw. Makono Brash ameuza mazao na ng’ombe mali ya mdai.
Hukumu hiyo imetolewa katika mahakama hiyo bila uwepo wa mdaiwa licha ya kutumiwa wito kufika mahakamani hapo mara mbili na hakufika. Hakimu Mbembela amesema mdaiwa hakuwahi kufunga ndoa na walitengana tangu mwaka 2008 na katika maisha yao ya ndoa walipata watoto sita wanaoishi na mama yao.
Amesema ili mdai awe na uhuru huo, lazima kwanza uhusiano wa ndoa uvunjwe na mahakama kwa mujibu wa sheria. Mahakama hiyo imeona sababu zilizotolewa na mdai zinaangukia kwenye makosa ya ukatili wa kimwili na kisaikolojia, hivyo uhusiano wa ndoa umevunjika kiasi cha kutorekebishika.
Katika shauri jingine lilifikishwa katika mahakama hiyo jana, Watu watatu wa familia moja wakazi wa kamakuka Mnyagala wilayani Mpanda wameshtakiwa kwa kosa la shambulio la kudhuru mwili na kusababisha upotevu wa mali.
Imeelezwa mahakamani hapo na WP 9737 PC Elly Neema kutoka jeshi la polisi Mpanda mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Bw. Mkumbi Ramadhani Mumbi kuwa , washatakiwa hao ni  Nogi Kahindi, Shilinde Nogi na Joseph Nogi na walitenda kosa hilo tarehe 03 mwezi Oktoba mwaka 2015 usiku majira ya saa nane, walimvamia mlalamikaji Jitobelo Ngalula ambaye ni mfugaji, na kuanza kumshambulia kwa fimbo huku wakihoji kwa nini amekataa kuhama katika eneo analoishi na wakati huo huo akimiliki eneo hilo kwa miaka sita sasa.
Akitoa ushahidi mbele ya mahakama, Mlalamikaji Bw. Jitobelo Ngalula aliwajibu kuwa eneo hilo wamekabidhiwa na serikali na waliendelea kumshambulia na kumsababishia majeraha kichwani, mkononi na mguuni na kusababisha upiotevu wa fedha shilingi laki moja na elfu hamsini, na simu aina ya Tecno yenye thamani ya shilingi elfu themanini.
Amesema baada ya kushambuliwa ilimlazimu akimbilie porini baada ya jirani yake kufika eneo la tukio na kuhoji sababu za kumshambulia kwa fimbo.
Washtakiwa wote wamekana shtaka dhidi yao na kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe nane mwezi Machi mwaka huu, na mahakama hiyo imeruhusu dhamana ya ahadi ya shilingi laki tano kwa kila mmoja na endapo hawatatimiza masharti ya dhamana warudishwe rumande hadi tarehe iliyopangwa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA