MKUU WA WILAYA MPANDA ATOA SIKU SABA KWA OFISI YA MADINI KUTATUA MGOGORO KATI YA KAMPUNI YA KIJANI INVESTMENT NA WACHIMBAJI WADOGO MPANDA.


Na.Meshack Ngumba-Mpanda
MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bwana  Pazza Mwamlima ametoa siku saba Kwa ofisi ya Madini Wilayani Mpanda Kutatua Mgogoro uliopo baina ya Kampuni ya Kijani Investment na Wachimbaji wadogo wa dhahabu Katika Machimbo ya Dilifu.
                                            
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw.Pazza Mwamlima Akizungumza na wananchi waishio katika mgodi wa dhahabu wa Dirifu ambao kipato kikuu wanategemea mgodi huo (PICHA NA Issack Gerald)

Akizungumza jana Katika Mkutano wa hadhara na Wakazi wa Kijiji cha dilifu kilichopo Katika Kata Manga Mwamlima amewata wachimbaji hao kuendelea na shughuli za Uchimbaji wakati Malalamiko yao yakitafutiwa ufumbuzi.
Uamzi huo umetolewa ikiwa ni siku Moja baada ya wachimbaji wadogo Katika Machimbo hayo Kuanzisha Maandamano yasiyokuwa na kikomo kufuatia ofisi ya Madini Mkoani Katavi  Kusitisha shughuli za Uchimbaji  kuendelea Katika Machimbo hayo kwa madai ya Kukosa  leseni ya Uchimbaji.
Hata hivyo wachimbaji hao wameiomba Serikali Kushughulikia Migogoro iliyopo baina ya wawekezaji na Wachimbaji wadogo wadogo inayochangiwa na Kuwepo kwa baadhi ya watumishi wasio waminifu Katika sekta ya Madini hapa nchini.
Mbali na wachimbaji wa dirifu,pia kumekuwepo malalamiko ya wachimbaji wapatao 200 katika mgodi wa dhahabu uliopo mlima wa Kampuni wakilalamika kufukuzwa katika mgodi huo wakati eneo hilo ndilo tegemeo la takribani miaka 36 iliyopita yaani miaka ya 1980.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA