BENKI YA DUNIA KUFADHIRI UJENZI WA KILOMITA 7.7 ZA BARABARA MANISPAA YA MPANDA 2016/2017


Na.Issack Gerald-Mpanda
Zaidi ya kilometa 7.7 za barabara katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ,zimetengwa kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami  kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
                                          
Benki ya dunia

Taarifa ya ujenzi wa barabara hizo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Bw.Hamis Mkele, wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Sambamaba na Mpanda Radio kwa njia ya simu.
Mkele amesema kuwa ujenzi huo unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu unadhaminiwa na  benki ya dunia.
Aidha amesema kuwa  amesema ujenzi wa barabara hizo hautafanyika kwa pamoja kutokana na fungu la fedha watakalopatiwa kutoka benki hiyo kutokuwa na uhakika kama litatosheleza mahitaji.
Baadhi ya Barabara hizo zinazotarajiwa kujengea kwa kiwango cha lami ni pamoja na barabara ya Afya Dispensal hadi Istiqama,Hospital ya Wilaya hadi Istiqama,kutoka Shule ya Sekondari St.Mary’s hadi madukani na barabara zinazozunguka eneo la mitaa ya Kashaulili.
Mara  kwa mara wakazi wa Manispaa ya Mpanda wamekuwa wakilalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara hali inayowapa taabu ya kupita kuelekea wanakohitaji kupatiwa huduma ikiwa ni pamoja na Hospitalini kutokana na barabara zilizo nyingi kutopitika hususani msimu wa masika.

Benki ya Dunia ni taasisi ya kimataifa yenye shabaha ya kusaidia maendeleo ya nchi za dunia. Si benki ya kawaida. Inashirikiana na Umoja wa Mataifa na hasa Shirika la Fedha la Kimataifa lakini si chini ya UM moja kwa moja. Ni mali ya nchi wanachama 185 zinazopigia kura katika mikutano yake kulingana na thamani ya hisa zao katika rasilmali ya benki.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA