MAFUNZO YA SIKU 3 KUHUSU UTUNZAJI WA FEDHA NA MALI ZA UMMA KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA YAANZA KATAVI.


Na.Issack Gerald-Katavi
MAHAKAMA ya Tanzania   imeanza  mafunzo ya siku 3  kuanzia leo hadi February 27 juu ya utunzaji wa fedha na mali ya umma kwa watumishi wa mahakama ya Tanzania mkoani Katavi katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mpanda.
                                                 

Mtendaji wa mahakama ya Tanzania mkoani Katavi Bw. Ipyana Isaac Kakuyu, amesema mafunzo hayo yamejumuisha watumishi wa kada za uhasibu, ugavi, utumishi pamoja na Teknolojia ya habari na mawasiliano -Tehama.
Amesema mafunzo haya yanalenga kuwajengea zaidi uwezo wa kuelewa masuala muhimu yanayohusu utunzaji wa fedha na mali ya umma pamoja na kanuni na taratibuza manunuzi kama ilivyoainishwa katika sheria ya fedha ya namba 6 ya mwaka 2001 iliyoboreshwa mwaka 2004 na sheria ya manununzi ya umma na.7 ya mwaka 2001 paoj ana kanuni na taratibu za manunuzi za mwaka 2013 ili kuongeza utdhibiti na uwajibikaji katika kusimamia.
Ametaja changamoto zinazowakabili kuwa ni uhaba wa watumishi wa kusimamia rasimali za umma, pamoja na kanuni na taratibu za manunuzi kukosekana katika mahakama ya mkoa wa Katavi .
Washiriki katika mafunzo hayo ni pamoja na Mkuu wa Hazina ndogo Mkoani Katavi,Mkaguzi Mkazi kutoka Ofisi ya taifa Mkaguzi na mdhibiti Mkuu Mkoani Katavi Bw.Philbert Kanyogozi,Mhakiki mali mwakili Mkoani Katavi Bw.Julius Mwanganikani,Hakimu mkazi mfawidhi Mkoani Katavi Mh.Chigangwa Tengwa,Mkaguzi wa ndani kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na wajumbe mbalimbali.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA