MAOFISA WA JESHI LA POLISI 458 WATIMULIWA KAZI
Jumla ya maofisa wa Jeshi la Polisi
wapatao 458 wamefukuzwa kazi kutokana na utovu wa nidhamu kuanzia mwaka 2015
hadi Machi mwaka huu.

Sirro alisema kazi ya Jeshi la Polisi
ni kurekebisha mienendo ya wananchi, hivyo kabla hawajawaelimisha wananchi
wanapaswa kuwa na mienendo mizuri wao kwanza.
Alifafanua kwa kulitambua hilo ndiyo
maana askari waliokwenda kinyume na azma hiyo walichukuliwa hatua ikiwa ni
pamoja na kufukuzwa kazi, ambapo kwa mwaka 2015, 198 walifukuzwa kazi.
Alisema kwa mwaka 2016 walifukuzwa
askari 165, 2017 (81) na kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu wamefukuzwa
askari 14.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments