WANAFUNZI KIDATO CHA NNE KATAVI WAMESEMA WATAFAULU MTIHANI
Na.Issack Gerald-Katavi

Wakizungumza
kwa nyakati tofauti,wanafunzi hao wakiwemo wa shule ya sekondari Mwangaza na Kashaulili
wamesema maandalizi yao katika mtihani huo yako vizuri huku wakiwaomba wenzao
kuondoa hofu ya mtihani.
Kwa
upande wake Mkuu wa shule ya sekondari Mwangaza Mwl.Simoni Lubange amewataka
wanafunzi wake kujiamini na kumtanguliza mungu katika ujibuji wa mitihani yao
kwa alichokisema hakuna kitu kigeni watakachokutana nacho.
Jumla
ya watahiniwa 385,938 wa kidato cha nne nchini wameanza mtihani leo huku baraza
la mitihani likitoa onyo kwa na tahadhari kwa wamiliki wa shule watakaofanya
udanganyifu.
Comments