ZITTO AMEMPONGEZA NYALANDU KUJIUDHURU NDANI YA CCM NA KUACHA UBUNGE

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo),Zitto Kabwe amempongeza Mbunge wa Singida Kaskazini(CCM), Lazaro Nyalandu kuwa ameonyesha uongozi uliokomaa.
Zitto ametoa maoni yake hayo baada ya Nyalandu kuamua kujiondoa CCM na kuachia nafasi yake ya ubunge.
Zitto ameandika, "Lazaro Nyalandu,umeonyesha uongozi. Kwa namna haki za watu zinavyovunjwa na uchumi wa nchi unavyoporomoka, unahitaji roho ngumu sana kuwa CCM.Umefanya maamuzi sahihi,wakati sahihi na kwa sababu sahihi. Kila la kheri."
Lazaro Nyalandu leo ametangaza kujivua nafasi zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuandika barua yake ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kwa kile alichodai kuwa Chama Cha Mapinduzi na Bunge vimekuwa vikishindwa kuisimamia serikali na badala yake kutumiwa na serikali jambo ambalo yeye anaona halina afya katika maendeleo ya nchi na linadidimiza haki mbalimbali. 

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA