MKUU WA WILAYA AIBULIWA NA SHULE KUITA WAGANGA KUTOKA KONGO


Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mohamed Mtanda ametolea ufafanuzi suala la shule ya Msingi Kabwe kuita waganga wa kienyeji kutoka Kongo ili kutatua tatizo la kishirikina linaloikabili shule hiyo.`
Mtanda amesema ni kweli alipokea simu kutoka kwa Mkuu wa shule hiyo kumuelezea matatizo yao hapo shuleni na lengo walilofikia serikali ya kijiji ili kutatua tatizo hilo ambalo limekuwa likijitokeza mara kwa mara.
Licha ya hayo,mkuu wa wilaya hiyo amesema yeye kama kiongozi wa serikali ni kulichukua tatizo hilo kitaalam kwa kupeleka madaktari ambao watatafuta njia sahihi ya kutibu wanafunzi hao na sio kuruhusu mambo ya kishirikina ingawa hawezi kuwakataza wazee wa kijiji hicho kwani anaheshimu mila zao.
Wanafunzi wa kike wa shule ya msingi Kabwe iliyopo Wilayani Nkasi mkoani Rukwa wanakabiliwa na tatizo la kiafya la kuanguka,kuzimia na kupiga kelele jambo ambalo wakazi wa eneo hilo wanahisi linatokana na ushirikina na kuamua kutafuta waganga wa kienyeji ili kutafuta ufumbuzi.
Chanzo:eatv
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA