IJUMAA KUU


Ijumaa Kuu ni siku maalumu ya mwaka ambayo wafuasi wengi wa Yesu Kristo wanaadhimisha kifo chake msalabani ambacho kilitokea nje ya kuta za mji wa Yerusalemu siku ya Ijumaa.
Kadiri ya Injili ya Mtume Yohane,kesho yake ilikuwa Sabato na pia Pasaka,jambo lisilotokea kwa kawaida. Kwa sababu hiyo wataalamu mbalimbali wanakadiria ilikuwa tarehe 7 Aprili 30.
Ijumaa kuu ni sehemu ya Juma Kuu linaloanza kwa adhimisho la Yesu kuingia mji huo akishangiliwa kama mfalme wa Wayahudi (yaani Masiya au Kristo).Adhimisho hilo linafanyika mwanzoni mwa wiki, yaani Jumapili ya matawi.
Ijumaa kuu ni pia sehemu ya siku tatu kuu za Pasaka zinazoadhimisha mateso na kifo chake (Ijumaa), kulala kaburini (Jumamosi), na hatimaye kufufuka kwa utukufu (Jumapili), kwa ufupi: Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka.
Jana ilikuwa Alhamisi KUU
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA