RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA MAAMUZI YA UN

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ameelezea kusikitishwa na uamuzi wa Umoja wa Mataifa kuanza kutekeleza sera ya kupunguza gharama kwenye misheni za kulinda amani.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati wakizungumza na mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa wanaziwakilisha nchi zao hapa nchini mkutano ambao umefanyika ikulu jijini Dar es salaam.
Amesema hatua hiyo itadhohofisha jitihada za kutafuta amani kwenye maeneo yenye migogoro na kuhatarisha maisha ya walinda amani pamoja na raia wasio na hatia wanaoishi kwenye maeneo yenye migogoro.
Wakati huo huo pamoja na mambo mengine Mhe.Rais Magufuli amesema pamoja na nia njema ya mpango wa majaribio wa kutafuta suluhu la kudumu ya tatizo la wakimbizi,Tanzania imeamua kujitoa kutokana na changamoto za kiusalama na ukosefu wa fedha za kugharamia mpango huo.
Wakati huo Rais Magufuli amesema Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wakiwemo wa kimataifa wote wanaohitaji kuwekeza hapa nchini.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA