MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AVUNJA BODI YA CHAMA WAKULIMA WA TUMBAKU MISHAMO TAMCOS



Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika
MKUU wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Saleh Mbwana Mhando,ameivunja bodi ya chama cha wakulima cha tumbaku MISHAMO TAMCOS na kuamru viongozi wote wa bodi hiyo wakamatwe haraka.
                                            

Wakulima wa Chama cha Ushirika Mishamo Tamcos katika picha wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika pichani hayupo

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mbwana Mhando akizungumza na wakulima wa chama cha Ushirika MISHAMO TAMCOS(Picha na Issack Gerald)


Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha MISHAMO TAMCOS Bw.Bw.Pridas Amakredo(picha na Issack Gerald)


Mkuu wa Wilaya ametoa agizo hilo kufuatia tuhuma za upotevu wa zaidi ya Shilingi milioni 140 kwa ajili zilizokatwa kwa wakulima kwa ajili ya upandaji miti ambapo hata hivyo miti hiyo haikupandwa.
 ’Naanza na Yule wa kwangu,Afisa ushirika,Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda,nilimuuliza mara tatu akaniambia uongo,nilimtuma hakutekeleza,huyu mtumishi wa umma kwenye wilaya ya Tanganyika hana nafasi,na kwa utaratibu wa serikali ya awamu hii ya awame ya tano tunasema kwamba,mtumishi wa umma akiharibu hahami anafia hapohapo’’alisema Mbwana Mhando.
Wakati huo huo mkuu wa Wilaya alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda,kumsimamisha kazi Afisa Ushirika Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Luxford Mbunda kwa kushindwa utekeleza wajibu wake na kuidanganya serikali. 
MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Bw.Saleh Mbwana Mhando,Septemba 15 mwaka huu wakati akizungumza na wakulima wa chama cha msingi cha ushirika cha MISHAMO TAMCOS aliuagiza uongozi wa bodi ya Chama cha Msingi cha Ushirika TAMCOS na Afisa Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Luxford Mbunda,kuhakikisha wanalipa  zaidi ya Shilingi milioni 200 zikiwemo hizo zaidi ya shilingi milioni 140 za upandaji miti ambapo wakulima hao walidai kuwa wakulima wa zao la tumbaku wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika hawajalipwa kwa misimu 3 ya kilimo kuanzia mwaka 2011-2015 ambapo bodi hiyo ilitakiwa ilipe kiasi hicho kabla ya Septemba 30 mwaka huu.
Miongoni mwa viongozi wanaunda bodi ya chama hicho ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Ushirika TAMCOS Bw.Pridas Amakredo.
Bodi hiyo imevunjwa juzi
Habari hii pia ipate kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri au ukiwa na habari yoyote tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA