SHIRIKA LA UNHCR KESHO KUKABIDHI GARI KWA JESHI LA POLISI MKOANI KATAVI KUSAIDIA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA



Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi
SHIRIKA la wakimbizi duniani UHNCR Mkoani Katavi,kesho linatarajia kukabidhi gari kwa jeshi la Polisi Mkoani Katavi ili kurahisisha shughuli za ulinzi na usalama za jeshi hilo.
                                          

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari,Afisa habari wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi Bw.Danny Kimario amesema kuwa makabidhiano hayo yanatarajiwa kufanyika katika makazi mapya ya Mishamo yaliyopo katika kata na Tarafa ya Mishamo Wilayani Tanganyika ambapo katika eneo hilo pia zipo Ofisi za UNHCR.
Mwaka uliopita,jeshi la polisi mkoani Katavi lilieleza kuwa na upungufu wa magari hali inayopelekea baadhi ya shughuli za jeshi hilo kukwama.
Shirika la wakimbizi duniani UNHCR mbali na tukio hilo linalotarajiwa kufanyika kesho,UNHCR pia  limekuwa likisaidia vitendea kazi katika sekta mbalimbali zikiwemo  elimu,afya na sheria ambapo katika sekta ya afya, hivi karibuni walikabidhi gari la kuhudumia wagonjwa  lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 78 katika kituo cha afya Mishamo.
Endelea kuwa name kufahamu kitakachojili kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA