BARAZA LA MADIWANI HALMSHAURI YA WILAYA YA MPANDA KUFANYA KIKAO CHAKE KESHO,SHILINGI MIL.120 ZILIZOTUMIKA KINYUME NA MALENGO,BARAZA LA MADIWANI KUTOA TAMKO



Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi
BARAZA la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi,kesho linatarajia kufanya kikao chake cha robo ya mwaka kwa mwaka 2016 ambapo masuala mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo kutoa  tamko la kubadilishwa matumizi ya Shilingi milioni 120 zilizokuwa zitumike kununulia gari la Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri hiyo ambapo zilitumika kwa ajili ya Masuala ya mitihani.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Hassan Mapengo(PICHA NA.Issack Gerald)
                                                

Katika mahojiano maalumu na mtandao huu leo,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh.Hamad Hassan Mapengo amesema pia kikao kinatarajia kujadili  taarifa za kamati mbalimbali za Halmshauri ili kuchanganua namna ya kutatua matatizo yanayokwamisha maendeleo kwa wananchi.
Aidha amesema awali walipanga na kupitisha bajeti ya kutumia shilingi milioni 150 kununua gari la mkurugenzi ambapo kiasi cha shilingi milioni 120 zilizokuwa zimepatikana baada ya kuuza magari mabovu na mali nyingine za  Halmshauri hiyo zikatumiwa bila baraza la madiwani kushirikishwa ambapo amesema baraza litatoa kauli juu ya pesa hiyo haraka ili kufanikisha ununuzi wa gari la Mkurugenzi mtendaji.
Wakati huo huo amesema,kabla ya kikao cha kesho,leo kumefanyika vikao vya kichama ili siku ya kesho kuwepo maamuzi katika masuala mbalimbali yanayomhusu mwananchi.
Kamati za kudumu za Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda ambazo zitawasilisha taarifa zake na kujadiliwa na baraza la madiwani ni pamoja na kamati ya fedha,uongozi na mipango,taarifa ya kamati ya elimu afya na maji,taafrifa ya kamati ya ujenzi,uchumi na mazingira sambamba na kamati ya Ukimwi.
Endelea kuwa name kufahamu kitakachojili kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA