MWALIMU WILAYANI MLELE AHUKUMIWA JELA MIAKA 30 KWA KUSABABISHA UJAUZITO KWA MWANAFUNZI WAKE



Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imemhukumu Mwalimu wa Shule ya Msingi Ukingwamizi, Une Thom kutumikia kifungo cha miaka 32 jela.

Thom (32) amehukumiwa kifungo hicho baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani kwa makosa mawili ya kumnajisi na kumpatia ujauzito mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 16.
Msichana huyo ambaye amejifungua mtoto njiti amefariki  baada ya kuzaliwa.
Kwa mujibu wa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Teotimus Swai  amesema kwa kuwa adhabu hizo zinaenda sambamba, mshitakiwa atatumikia kifungo cha miaka 30 jela.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Swai amesema mahakamani hapo kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ukiongozwa na Mkaguzi wa Polisi, Baraka Hongoli umethibitisha kuwa kweli mshtakiwa alitenda kosa hilo.
Mwendesha mashitaka, Mkaguzi wa Polisi, Baraka Hongoli amedai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi wake huyo kwa muda mrefu hadi akamsababishia ujauzito.
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au Ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA