TANESCO NA UFAFANUZI WA TATIZO LA UMEME MPANDA KATAVI



Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
Uchakavu na ubovu wa mitambo ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa katavi ndiyo imeelezwa kuwa ndio chanzo kinachosababisha kutokuwa na umeme wa uhakika.
Meneja mahusiano wa
shirika hilo mkoani Katavi Amon Michael amesema tatizo hilo litaendelea kuwepo hadi umeme wa msongo mkubwa na mitambo mipya itakapowasili na kufungwa.
Bw.Michael amesema uzalishaji wa umeme kwa mkoa ni kilowatt 3200, huku matumizi ya mkoa ikiwa ni kilowatti 2700 hivyo inapotokea mashine moja ikashindwa kufanya kazi, umeme unakuwa wa kusuasua.
Aidha Bw.Michael amewataka wananchi kutumia mafundi wa umeme wanaoshauriwa na shirika hilo ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kwa kutumia mafundi ambao hawajasajiliwa.
Hivi karibubi nyumba Moja iliungua kwa moto kutokana na hitilafu ya umeme ambapo hata chanzo chake hakijafahamika.
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au Ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA