JIMBO LA MPANDA MJINI LAPATA MGAO WA MADAWATI 537 KUTOKA MFUKO WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.



Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda
JIMBO la Mpanda mjini Mkoani Katavi limepatiwa mgao wa madawati 537 kutoka mfuko wa ofisi ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yamebainishwa jana Oktoba 14na Mbunge wa Jimbo hilo Mh.Sebastian Simon Kapufi wakati akihututubia wakazi wa kata ya Mpanda Hotel katika mkutano wa hadahara.
 Amesema kuwa mara baada ya kuletwa madawati hayo ambayo kwa sasa yapo Sumbawanga Rukwa mara baada ya kuwasiliwhwa Jimboni yatagawiwa kwa shule zenye upungufu wa madawati.
Katika hatua nyingine Mbunge Mh.Kapufi ametoa msaada wa Zaidi ya shilingi milioni mbili kwa makundi tofauti yaliyopo Kata ya Mpanda Hotel.
Misaada hiyo ambayo imetolewa na Mbunge ni pamoja na Shilingi Milioni 1 kwa ajili ya ukarababti mabomba ya maji Mpanda Hotel huku fedha nyingine ikitotolewa kwa makundi ya wapepeta pumba za mchele waliopatiwa Shilingi 500,000/=,na wagonwa wengine ambao wamepatiwa fedha taslimu kuanzia shilingi elfu kumi na tatu hadi laki mbili(13,000/= hadi 200,000/=.
Wakati huo huo huo suala la tatizo la maji,umeme na migogoro ya ardhi imetajwa na wananchi kuwa kikwacho cha maendeleo ya wananchi.
Hata hivyo juzi Oktoba 13,2016 katika kikao cha baraza la madiwani Manispaa ya Mpanda kulijadiliwa mikakati inayofanyika namna ya kutatua matatizo ya maji,umeme na migogoro ya ardhi katika Maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mpanda.
Jimbo la Mpanda Mjini lina Jumla ya kata zipatazo 15.
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Mawasiliano : p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA