MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AKAZA MWENDO KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA WILAYA YAKE



Na.Issack Gerald Bathromeo-Tanganyika
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh.Saleh Muhando ameahidi kulishughulikia swala la mgogoro wa ardhi katika eneo la Lyamgoroka eneo ambalo linaonekana kuwa limeuzwa na  mwenyekiti wa kijiji hicho   kinyume cha sheria ya ardhi.

Mkuu huyo wa wilaya amesema tayari serikali yake imeshachukua hatua ya kuwahamisha watu ambao walikuwa wakiishi katika eneo hilo kinyume cha sheria kwa kuwatafutia maneo mapya ya kuishi.
Aidha mkuu wa wilaya ya Tanganyika amewataka watumishi wote wa wilaya ya Tanganyika kuwa wadirifu punde wanapotoa huduma kwa jamii bila kupokea au kutoa rushwa kwani rushwa ndio adui namba moja wa maendeleo .
Katika hatua nyingine amewataka wafanyakazi wanaohodhi ardhi kinyume cha sheria kuacha mara moja kwani uongozi wa wawmu hii ni tofauti na wanatakiwa wasome alama za nyakati
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo-Mpanda
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA