WANAUME WATAJWA KUWA MIONGONI MWA SABABU ZINAZOCHANGIA KUONGEZEKA VVU KATAVI



 Na.Richard Sokoni-Mpanda
Imebainika kuwa  ongezeko la  maambukizi ya virus vya ukimwi (VVU) kunatokana  na  baadhi ya mwanaume  kutojitokeza kupima afya zao sanjari na wenzi wao .

Hayo yamesemwa na Afisa tathmini wa   mipango na ufutiliaji wa maambikizi ya ukimwi pamoja na magonjwa sugu katika shirika la shdepha mpanda Michael Kapipiti wakati wa mahjiano na mwandishi wetu ofisini kwake kuhusiana na mwamko wa jamii kuhusu kupima afya zao .
Aidha Bw.Kapipiti amesema kuwa baadhi ya wanaume bado hawana elimu ya kutosha kuhusu maambukizi ya virusi vya ukimwi na ukimwi wenyewe jambo ambalo linasababisha ongezeko la maambukizi ya ukimwi katika jamii.
Sanjari na hayo Bw. Kapipiti amesema kuwa wazazi na walezi wanapaswa kutoa elimu katika  familia zao ili kuwa na uelewa sahihi kuhusu maambukizi ya virus vya ukimwi  na ukimwi wenyewe 
Mmoja wa wakazi wa kata ya Makanyagio Bw. Kulwa Mabula amekiri  baadhi ya wanaume kutokuwa na desturi ya kupima na kujua afya  zao.
Mpaka sasa Mkoa wa Katvi takwimu ya maambukizi kwa mjibu wa tafiti za mwaka 2011/2012 ni asilimia 5.9 ambapo kuanzia kipindi hicho cha tafiti mpaka sasa inakisiwa idadi ya waathirika kuongezeka kutokana na idadi ya watumiaji dawa ya kufubaza VVU kuongezeka katika vituo vya afya vinavyotoa huduma hiyo.
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo-Mpanda
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA