KUTOKA WILAYANI MLELE KATAVI -TUKIO LA NYUMBA KUCHOMWA MOTO

Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama –Mlele Katavi
NYUMBA za wakazi ambazo idadi yake haijafahamika eneo la Namba moja lililopo Kata na Tarafa ya Inyonga Wilayani Mlele Mkoani Katavi,leo zimeteketezwa kwa moto na baadhi ya mali zilizokuwemo kuteketezwa katika nyumba hizo.
Kwa mjibu wa baadhi ya wakazi ambao mali zao zimeteketea ,wakizungumza na Mpanda Radio Kwa njia ya Simu kwa masikitiko makubwa akiwemo Bi.Tatu Masanja wamesema kuwa, tukio hilo ambalo wameliita la kushtukiza asubuhi ya leo,wamedai limetekelezwa na askari Mkoani Katavi kuanzia majira ya asubuhi.
Wametaja baadhi ya mali zao ambazo zimechomwa kwa moto mbali na nyumba zao kuwa ni pamoja na Vyakula na mavazi huku watoto wakizagaa ovyo katika eneo hilo bila wazazi wao baada ya wazazi kukimbilia kusikojulikana kufuatia wengine kupigwa na askari hao.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP damasi Nyanda,akizungumza na Mpanda Radio Kwa njia ya Simu mchana wa leo,amesema hajapata taarifa ya utekelezwaji wa tukio la uchomaji makazi ya watu na ameahidi kufutailia ukweli wa tukio hilo.
Hata hivyo,Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bi.Rachel Kasanda ambaye pia ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Wilayani Mlele amesema,hawezi kuzungumzia tukio hilo kwa kuwa lipo nje ya mipaka yake ya utawala isipokuwa akaongeza kuwa anachofahamu uchomaji wa nyumba hizo unafanywa na askari wa wanyama pori ili kuwaondoa wavamizi wa maeneo ya hifadhi eneo hilo ambalo ameliita kuwa siyo makazi halali ya watu bali ni hifadhi.
Hata hivyo juhudi za kuwatafuta TANAPA Mkoani Katavi zinaendelea ili kutolea ufafanuzi wa tukio hilo.
Tukio la kuchomwa kawa makazi ya watu Mkoani Katavi siyo la mara ya kwanza ambapo tukio linguine lilitekelezwa mwaka 2013 eneo la Luhafe lililopo makao makuu ya Wilaya ya Tanganyika Kata ya Majalila wakati huo ikiwa Wilaya ya Mpanda ambapo wakazi wa eneo hilo walidai kuchomewa nyumba na vyakula vyao pamoja na mali nyingine.
Endelea kuwa nami kupata ukweli wa tukio hilo kwa undani zaidi.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni,ushauri au ukiwa n ahabari yoyote,tutumie kupitia email ya Ofisi p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA