GEREZA LA KALILANKULUKULU NA TAASISI ZAKE AMBAZO NI SHULE NA ZAHANATI HATARINI,BAADHI YA WAFUNGWA HAWANA SARE,BAADHI YA ASKARI MAGEREZA NAO WALAZIMIKA KUTUMIA PESA ZAO KUSHONA SARE KWA MIAKA 8 SASA,KUTA ZA MAJENGO YA ZAHANATI NAYO KUANGUKA MUDA WOWOTE,VYOO VYA WANAFUNZI NAVYO VYAJAA VYAZIBA BILA HATUA KUCHUKULIWA KIPINDUPINDU KUBISHA HODI.



Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika Katavi
GEREZA la Kalilankulukulu lililopo Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi lililoanzishwa mwaka 1973 ,linakabiliwa na matatizo mbalimbali yakiwemo baadhi ya wafungwa wa gereza hilo kukosa sare huku pia baadhi ya asakari wa gereza hilo,wakilazimika kutumia pesa yao kushona sare zao kutokana na serikali kutowapa sare hizo tangu mwaka 2009 licha ya viongozi kadhaa wa wizara,Mkoa hadi Wilaya kuwa na taarifa ya matatizo hayo.  
Mwigulu Nchemba waziri wa mambo ya ndani ya Nchi ambaye kwa kiasi kikubwa gereza zipo chini ya wizara yake kama waziri
                                                              
Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe Naibu waziri wa Nishati na madini(Mbunge wa Jimbo la Katavi)
                      

Hali hiyo ya kukosekana kwa sare za wafungwa imethibitishwa na Mkuu wa Gereza la Kalilankulukulu ACP Samwel Oberthe  katika ziara ya kushtukiza ambayo imefanywa leo na mbunge wa viti maalumu  Mkoani Katavi Taska Mbogo,katika ziara ambayo alikuwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mhando huku tatizo la askari magereza kutumia pesa yao likithibitishwa na baadhi ya askari magereza ambao hawakutaka majina yao yatajwe.
Aidha Katika ziara hiyo,Mkuu wa Gereza la Kalilankulukulu ACP Samwel Oberth amezitaja changamoto nyingine zinazolikabili gereza hilo kuwa ni ukosefu wa umeme,maji ambapo wafungwa hualzimika kuchota maji tena yasiyo salama katika maenewo ya kona Mnyagala umbali wa kilomita 8 huku changamoto nyingine ya gereza hilo ikiwa ni hali mbaya uchakavu wa majengo ya gereza hilo.
Wakati huo huo ACP Oberthe amesema majengo ya zahanati ya Kalilankulukulu yapo hatarini kuanguka kutokana na kuwa na nyufa kubwa za muda mrefu ambapo huenda muda wowote kukatokea madhara makubwa kwa watumiaji wa majengo ya zahanati hiyo.
Nao baadhi ya wafungwa wakizungumza mbele ya mbunge wameeleza kusikitishwa na kutopata nakala za hukumu zao kwa muda mrefu na kutopata mrejesho wa rufaa wanazokuwa wamekata ambapo Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Mkuu wa Gereza wameahidi kufuatulia ili wafungwa wapate majibu yao kwa mjibu wa sheria.
Katika hatua nyingine Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kalilankulukulu Boazi Masoko,akizungumza katika ziara ya mbunge huyo amesema,matundu ya vyoo 5 vya shule hiyo yanayotumiwa na wanafunzi wapatao 500 yamejaa na kuziba tangu mwaka jana,ambapo hali hiyo inatishia muda wowote kutokea  milipuko wa magonjwa ya kipindupindu ikiwa serikali na wadau hawatachukua hatua za haraka kunusuru hali hiyo.
Kwa mjibu wa taarifa ya mkuu wa Gereza,kwa mwaka 2016 miongoni mwa viongozi waliopata na taarifa ya changamoto za gereza hilo ikiwemo baadhi ya  wafungwa kutokuwa na sare ni Pamoja na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh.Mwigulu Nchemba ambaye alipata taarifa alipofanya ziara Mkoani Katavi mwaka huu,huku changamoto ya ukosefu umeme akipewa naibu waziri wa nishati na Madini.
Katika changamoto ya Ukosefu wa maji,wizara ilipata taarifa kupitia kwa naibu waziri wa maji na umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe (Mbunge Jimbo la Katavi) ambapo viongozi wote kwa pamoja kwa nyakati tofauti waliahidi kuzifanyika kazi.
Hata hivyo,agizo la kupelekwa umeme katika gereza la Kalilankulukulu alilolitoa naibu waziri wa nishati na Madini kwa mwezi Agosti mwaka huu kwa Shirika na umeme Tanzania TANESCO Mkoani Katavi ,halijatekelezwa licha ya shirika hilo kusikika kupitia vikao mbalimbali likitoa taarifa ya mkakati wa umeme Mkoani Katavi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mhando amesema lazima matatizo ya gereza hilo hususani zilizopo chini Wilaya yake hatua za ufumbuzi zianshwe ambapo kwa Upande wake Mbunge Taska Mbogo mbali na kuahidi kuwasilisha matatizo ya wafungwa wa gereza hilo Bungeni pia ametoa msaada wa Zaidi ya laki tatu kwa ajili ya kununua vyombo kwa ajili ya kulia vyakula ambapo tatizo hilo nalo limekuwepo kutokana na kuongezeka kwa wafungwa kutoka 45 miaka iliyopita hadi 176 kwa sasa.
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA