MIFUGO KUZAGAA MITAANI KWAPIGWA WILAYANI KIBONDO



Na.Mwandishi wetu- Jastini Cosmas-Kibondo Kigoma
HALMASHAURI ya wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma,imewaagiza wananchi katika Halmshauri hiyo kutoachia mifugo yao ovyo katika kipindi hiki cha msimu wa kilimo,kutokana na mifugo hiyo kuwa waharibifu wa mazao.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kibondo Bw.Simoni Kanguye katika kikao cha baraza la madiwani wa halmshauri.
Aidha Kanguye,amewataka watendaji wa kata kuhakikisha kila mfugaji anaidhibiti mifugo yake ipasavyo.
Wakati huo huo Bw.Kanguye ameongeza kwa  kusema kuwa atakayebainika kuachia mifugo ovyo na kusababisha kuharibu mazao, atachuhukuliwa hatua kali za kisheria ikiambatana na faini.
Katika kutekelezwa kwa agizo hilo,maafisa watendaji wa Kata na Vijiji wameagizwa kusimamia zoezi la kutozagaa kwa mifugo ya wananchi na kuhakikisha wananchi wanazingatia maagizo ya Halmashauri.
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA