MKUU WA WILAYA TANGANYIKA:ENEO LA LUHAFE SASA KUJENGWA MJI WA MAKAZI NA BIASHARA.


Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika
MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando,ametangaza wakazi wa eneo la Luhafe lililopo kata ya Majalila,kulitumia eneo hilo kwa makazi na shughuli za kibiashara baada ya mgogoro wa uhalali wa eneo hilo wa muda mrefu.

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Saleh Mbwana Mhando akihutubia wakazi wa kitongoji cha Luhafe(PICHA NA.Issack Gerald)Septemba 16,2016 


                                                                        


Mkuu wa Wilaya ametangaza uamuzi huo jana,wakati akizungumza na wakazi wa eneo hilo ambao walitakiwa kuondoka tangu mwaka 2013 wakidaiwa kuvamia eneo hilo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya uwekezaji.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka wakazi wote waliovamia katika maeneo ya vyanzo vya maji kujiondoa wenye kabla ya Oparesheni ya kuwaondoa kwa nguvu mwezi ujao wa Oktoba mwaka huu ambapo miongoni mwa wanaotakiwa kutoweka na kusogea eneo la Luhafe ni pamoja na waliopo eneo la Ijamba palipo na mto Sabaga,Western,Misanga na Bariadi.
Kwa mjibu wa taarifa ya kitongoji hicho ambayo imesomwa kwa mkuu wa Wilaya,eneo la Luhafe lina wakazi wapatao elfu tatu wanaofanya shughuli ya kilimo na ufugaji.
Kwa Upande wake Afisa Mipango miji na Vijiji katika Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw.Elisha Mengele,ametoa wito kwa uongozi wa eneo la Luhafe kuendesha sensa ya kubaini idadi ya watu ili viwanja vipimwe na hatimaye kuanza kujenga makazi ya kudumu baada ya kushidwa kufanya hivyo wakihofia kufukuzwa.
Naye Filbert Kombe Nguvumali ambaye ni afisa elimu taaluma Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika,amesema kwa sasa mpango uliopo ni kujenga shule za kudumu kwa ajili ya wanafunzi wapatao zaidi ya 931 kuanzia chekechea hadi darasa la sita waliopo katika vituo vinavyotumika kufundisha wanafunzi ambapo vituo hivyo vilikuwa havitambuliki kwa serikali.
Hata hivyo wakazi hao walidai kuwa mwaka 2013 walichomewa nyumba zao na mali zilizokuwemo wakati wa uendeshaji wa Oparesheni Tokomeza ujangili.
Kwa upande wao wananchi wamepokea kwa furaha tangazo la serikali kuwaruhusu kuishi mahali hapo wakati mipango miji ikifanyika na hatimaye kuendesha shughuli za biashara bila kikwazo.
Habari hii pia ipate kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri au ukiwa na habari yoyote tuma kupitia p5tanzania@gmail.com


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA