NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO MPANDA



Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda
Moto umeunguza nyumba ya Familia moja na kusababisha hasara ya mali ambayo thamani yake haijajulikana katika mtaa wa Migazini kata ya Makanyagio  Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Mashuhuda wa tukio hilo Patrick Kapose na Elizabeth Matonge wamesema moto huo uliozuka majira ya mchana umesababishwa na hitlafu ya umeme.
Aidha,kwa mjibu wa mashuhuda,nyumba hiyo imeungua muda mfupi baada ya Shirika la Umeme Nchini Tanesco Mjini Mpanda kufunga mita mpya baada ya kuondoa mita ya zamani iliyokuwepo.
Kamanda wa zimamoto aliyeongoza uzimaji wa moto huo amewataka wananchi kutoa taarifa mapema mara tu majanga yanapotokea ili kuepusha athari zaidi. 
Habari hii pia ipate kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri au ukiwa na habari yoyote tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA