VIJIJI ZAIDI YA 14 VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO KUPATA UMEME WA REA AWAMU YA III MWAKA 2016

Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda,Katavi
Meneja wa TANESCO mkoa wa Katavi Mhandisi Julius Sabu amesema katika awamu ya tatu ya umeme wa REA wanampango wa kusambaza umeme katika vijiji ambavyo havikupitiwa na mpango huo katika awamu zilizopita.
                                   

Meneja huyo ametaja vijiji vitakavyonufaika na mradi wa REA wa awamu ya III kuwa ni Katumba,Mnyaki A,Mnyaki B,Kaminula,Soko nne,Tambaza A,Tambaza B,Ivungwe A,Ivungwe B,Nzanga,Iwimbi,Mtambo,Kalungu na Ndui Station.
Aidha Mhandisi Sabu amesema kuwa tatizo la kukatika kwa umeme maeneo mbalimbali ya mji wa mpanda inatokana na uchakavu wa mitambo ya kuzalisha nishati hiyo.
Kwa nyakati tofauti ,wakazi wa  Tarafa ya Katumba kwa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wilayani Mpanda Mkoani Katavi kwa Ujumla wamekuwa wamelalamikia hali ya kukosekana kwa huduma ya nishati ya umeme katika eneo lao.
Hata hivyo,kumekuwa na tatizo la kukati kakatika kwa Umeme Wilayani Mpanda kwa wakazi wa Mpanda Mjini wanaotengemea umeme wa Tanesco na hivyo kuathirika kiuchumi ikizingatiwa kuwa mbali na kuunguliwa kwa vifaa vya ndani pia,wakazi wengi wanakwama kuendesha biashara zinazotegemea umeme kama viwanda vya kukoboa na kusaga nafaka.
Habari hii pia ipate kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri au ukiwa na habari yoyote tuma kupitia p5tanzania@gmail.com


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA