MUWASA : WAKAZI MANISPAA YA MPANDA WANAKOSA MAJI KUTOKANA NA UPUNGUFU WA MAJI KUTOKA VYANZO VYA MAJI




Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi
MAMLAKA ya maji safi na salama Manispaa ya Mpanda MUWASA Mkoani Katavi imesema kuwa,tatizo la upatikanaji wa maji lililopo kwa sasa kwa wakazi wa Manispaa ya Mpanda,linatokana na upungufu wa kina cha maji katika vyanzo vinavyotoa maji.
Ikorongo Namba 2 chanzo cha Maji Manispaa ya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald)
                                

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa maji Mkoani Katavi Mhandisi Zacharia Nyanda wakati akijibu hoja za madiwani katika kikao cha baraza la madiwani Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda ambacho kimefanyika katika Ukumbi wa Idara ya Maji Manispaa ya Mpanda.
Mhandisi Nyanda amesema,kwa sasa kiwango cha maji kinachozaliswa kutoka vyanzo vya maji mbalimbali ni lita za ujazo Milioni tatu na laki moja na nusu huku mahitaji kwa wananchi yakiwa ni lita za ujazo Milioni 9.5 ambapo kiasi kinachohitajika kuzalishwa ili kumaliza tatizo ni lita milioni sita.
Aidha amesema katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo la maji Manispaa ya Mpanda,Mamlaka ya maji safi na salama MUWASA imekusudia kuongeza lita za ujazo lita milioni moja kwa mwaka huu.
Hata hivyo mbali na wakandarasi wanaotarajia kuanza mikakati ya kuweka miundombinu ya Maji Manispaa ya Mpanda,pia Mhandisi Nyanda amesema upo Mpango wa kuvuta maji kutoka ziwa na Tangamyika na kuboresha chanzo cha maji Ikorongo namba 2.
Miongoni mwa kata ambazo zimetajwa kukithiri kwa tatizo la maji kwa muda mrefu ni pamoja na kata za Mpanda Hoteli,Makanyagio,Kashaulili.
Hata hivyo maeneo mengi ikiwemo eneo la Madukani upungufu wa maji katika vyanzo vyua maji unatokana na mabomba yenye upana mdogo yanayopitisha maji kutoka vyanzo vya maji hadi kwa wananchi.
Endelea kuhabarika zaidi na P5 TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Mawasiliano kwa ushauri : p5tanzania@g,mail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA