MKUU WA WILAYA MPANDA AWAAGIZA WATUMISHI WENYE VYETI BANDIA KUJIONDOA WENYEWE KABLA YA KUKAMATWA,MANISPAA YA MPANDA NAYO YAAGIZWA KUWA NA NIDHAMU YA MATUMIZI YA BAJETI YA FEDHA ZA MAENDELEO.



Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi
MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi. Lilian Charles Matinga,amewaagiza watumishi wote wenye vyeti bandia Wilayani Mpanda kujiondoa wenyewe kwa hiari kabla ya kukamatwa na hatua kali kuchukuliwa dhidi yao.
MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Charles Matinga(Asiyevaa wigi)
Mh.Sebastian Mwakabafu Diwani wa kata ya uwanja wa ndege katika kikao akiuliza swali
                               

Mkuu wa Wilaya ametoa agizo hilo leo katika kikao cha baraza la madiwa Manispaa ya Mpanda ambacho kimefanyika katika Ukumbi wa Halamshauri ya Manispaa ya Mpanda.
Licha ya kuwa Mkuu wa Wilaya hakutaja idadi ya watumishi wenye vyeti badia Wilayani Mpanda,Bi.Matinga amesema mpaka sasa wakati zoezi la ukaguzi likiendelea kuna baadhi ya watumishi wenye vyeti bandia wamekwishainika.
Hivi karibuni serikali iliagiza nchi nzima kupitisha msako wa kuhakiki vyeti vya watumishi wote wa umma wenye vyeti bandia ili waondolewe katika utumishi.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ametoa agizo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha za bajeti kwa ajili ya maendeleo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kila bajeti inapopangwa.
Amesema kuwa ni lazima matumizi ya fedha za serikali yazingatiwe kwa kuwa fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Wakati huo huo amesema kila mtumishi Wilayani Mpanda  anatakiwa kuepuka vitendo vya rushwa,kutouza mali za raia kujinufaisha mwenyewe kwa kivuli cha kuwa kiongozi huku pia watumishi wakitakiwa kuzingatia mipaka ya mamalaka ya majukumu yao kuepusha mwingiliano wa majukumu kati ya idara moja na nyingine.
Kikao cha leo ambacho ni cha kwanza kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kimehudhuriwa pia na Mbunge wa jimbo la Mpanda Kati Mh.Sebastian Simon Kapufi  na Mbunge viti maalum mkoani Katavi Mh.Rhoda Kunchela.
Endelea kuhabarika zaidi na P5 TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA