KIFO CHA MTU KUJINYONGA KATAVI,NDUGU,MASHUHUDA WASIKITIKA


Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
MTU mmoja anaekadiliwa kuwa na umri wa miaka 30 Innocent Milambo mkazi wa mtaa wa kigoma kata ya Makanyagio wilayani Mpanda  mkoani Katavi,amekutwa amekufa kwa kujinyonga  usiku wa kuamkia leo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda(PICHA NA.Issack Gerald)
                                                            

Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi ACP Damasi Nyanda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kwamba madaktari wanafanya uchunguzi katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda ili kubaini chanzo cha kifo hicho.
Aidha kamanda Nyanda ameitaka jamii kuacha kujiadhibu kwa kujichukulia sheria,mkononi kwani maamuzi yoyote ya kukatisha uhai ni kosa kisheria.
Nao baadhi ya ndugu,majirani pamoja mashuhuda wa tukio hilo,mbali na kueleza kusikitishwa na kifo cha Marehemu Innocent Milambo,wamedai kuwa huenda kuna watu wamehusika na kifo hicho kwa kuwa inadaiwa kuwa marehemu alianza purukushani nyumbani kwa kuwatishia kuwapiga waliokuwepo.
Habari hii pia ipate kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri au ukiwa na habari yoyote tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA