MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA ATOA AGIZO KWA WATUMISHI WA WILAYA HIYO,ATAKA WAFANYE KAZI KWA WELEDI KWA MANUFAA YA WANANCHI NA KUIEPUKA RUSHWA.


Na.Issack Gerald Bathromeo-Tanganyika Katavi
MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Saleh Mbwana Mhando,amewaagiza watumishi wa umma Wilayani Tanganyika,kufanya kazi kwa weledi na kasi ili kufikia maendeleo yanayohitajika kwa wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika(Mwenye tai) akiwa na baadhi ya watumishi wa Wilaya hiyo baada ya kikao(PICHA NA.Issack Gerald)Septemba 14,2016
Baadhi ya watumishi wa idara mbalimbali halmashauri ya wilaya ya Tanganyika katika kikao cha utumishi na mkuu wa Wilaya(Hayupo pichani)(PICHA NA.Issack Gerald)Septemba 14,2016
                                          

Bw.Muhando ametoa agizo hilo leo,wakati akizungumza na watumishi wa idara mbalimbali wa Wilaya hiyo,ambapo amewataka kujiepusha na vitendo vya Rushwa vinavyopelekea kukwamisha kukamilika kwa miradi ya maendeleo kwa wakati.
Wakati huo huo,Bw.Mhando pamoja na kutaka utatuzi wa matatizo ya wananchi ulenge katika sekta nyeti ikiwemo huduma ya maji,afya na elimu pia amewaagiza wakuu wa idara za kilimo kuelekeza nguvu nyingine katika uanzishwaji wa miradi mingine ya maendeleo itakayoongeza kipato cha Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika huku katika hatua akiitataka idara ya misitu ifanye kazi yake ya kukamata wanaoharibu mazingira kwa kukata  na kuchoma misitu na ovyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Mpanda Bw.Beda Katani ambaye pia ndiye kaimu mwenyekiti wa chama hicho Wilayani Tanganyika,pamoja na kuiomba serikali kuboresha maslahi ya watumishi kuendana na hali ya maisha kwa sasa yanavyopanda gjharama,amesema chama kitashirikiana na serikali ipasavyo kuleta maendeleo ya wananchi ikiwemo kuwafichua wanaokwamisha maendeleo.
Hata hivyo,kwa mjibu wa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Saleh Mbwana Mhando, pamoja na kusema kuwa kikao cha leo kilikuwa cha kupeana mwelekeo wa namna ya kuleta maendeleo wilayani Tanganyika kwa kila mkuu wa Idara kwa kuzingatia mahitaji ya mwananchi,pia amesema,hivi karibuni anatarajia kufanya kikao baina yake na  madiwani wa Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika ili kuelezana namna ya kukamilisha ahadi za serikali ya awamu ya tano katika wilaya hiyo,ikiwemo pia hata ahadi alizoahidi Rais Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwakajana katika mikutano mbalimbali wilayani humo ambazo hazijaandikwa katika ilani ya chama cha mapinduzi.
Habari hii pia ipate kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri au ukiwa na habari yoyote tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA